Habari za hivi punde, Polisi waapa kuwanasa waliomteka Mo Dewji
Polisi nchini Tanzania wamesema watafanya kila wawezalo kuwatia nguvuni watu waliomteka na kumshikilia bilionea Mohammed Deji, Mo, kwa siku tisa.
Mkuu wa jeshi hilo, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Simon Sirro amewaambia waandishi wa habari hii leo Oktoba 20 kuwa kuachiwa kwa Mo ni mwanzo wa kuwanasa wahalifu hao na kjuahidi kuwapata wakiwa wazima au wamekufa.
"Mbio ukizianza sharti uzimalize. Huu ni mwanzo tu. Hao wahalifu wanaotaka kuchafua jina la nchi yetu lazima tuwatie nguvuni."
Sirro amesema upelelezi umeimarishwa kwa kushirikiana na mtandao wa polisi wa kimataifa Interpol.
"Nataka niwaambie (wahalifu) yawezekana wananisikiliza hivi sasa kuwa, popote watakapoenda tutawanasa. Wakienda Afrika Kusini tunao, Kenya tunao, Uganda tunao hata Msumbiji, popote pale tutawakamata maana tayari tunaushirikiano na wenzetu."
Fuatilia habari hii zaidi hapa: https://www.bbc.com/swahili/habari-45927232