Euro 2024: England kukutana na Hispania katika fainali
Hispania imekuwa timu iliyosisimua zaidi katika mashindano na walikutanishwa na timu nzito katika droo ya mashindano haya. Katika awamu ya makundi waliishinda Italia Albania na Croatia kuongoza katika kundi hilo.
Hii iliwasukuma kukutana na Georgia katika awamu ya timu 16 ambapo waliifunga timu hiyo 4-1.
Katika robo fainali waliikaribisha Ujerumani na Dani Olmo alifunga bao la kwanza kabla ya Florian Wirtz kulisawazisha kunako dakika 89. Mikel Merino alilisukuma tobwe la ushindi katika muda wa ziada na kuipatia timu hiyo fursa ya kuingia katika nusu fainali dhidi ya Ufaransa.
Katika kinachotajwa kuwa mechi bora zaidi. Mchuano kati ya Uhispania na Ufaransa ulisisimua.
Randal Kolo Muani aliifungia Ufaransa bao la utangulizi lakini mawili ya haraka kutoka Lamine Yamal na Olmo yaliipatia Uhispania ushindi.
Sasa ni England tu ndio kizuizi kwa miamba hiyo ya Uhispania kunyakua ubingwa.
Safari ya England kueleka fainali Haijakuwa safari rahisi kwa England kufika katika fainali. Walianza kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Serbia kufuatia mkwaju wake Jude Bellingham.
Sare ya 1-1 dhidi ya Denmark alafu sare nyingine ya 0-0 dhidi ya Slovenia iliwafanya kuibuka kidedea katika kundi lao. Katika mechi ya timu 16 England ilikutana na Slovakia katika mechi ilioingia katika muda wa ziada.
Hatimaye Harry Kane alifanikiwa kufunga bao la ushindi. England ilifuzu katika robo fainali ambako ilikutana na Uswizina kupata ushindi wa 5-3 kupitia mikwaju ya penalti.
England ilikuwana kibarua kigumu katika nusu fainali ilipotuna na miamba ya soka Uholanzi.
Ollie Watkins alifanikiwa kufunga bao la ushindi katika dakika ya mwisho ya mechi hiyo. Sasa inapokutana na Uhispania katika fainali, msema kweli ni nani?
Unaweza kusoma;