Kwaheri hadi kesho
Na hapa ndio mwisho wa taarifa zetu za moja kwa moja, tukutane kesho.
Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Katika makubaliano yaliyosimamiwa na Umoja wa Falme za Kiarabu, Urusi imesema imetoa wanajeshi 150 wa Ukraine kwa idadi sawa ya wanajeshi wa Urusi.
Na Dinah Gahamanyi & Rashid Abdallah
Na hapa ndio mwisho wa taarifa zetu za moja kwa moja, tukutane kesho.
Urusi na Ukraine zimebadilishana mamia ya wafungwa wa kivita, imesema wizara ya ulinzi ya Urusi.
Katika makubaliano yaliyosimamiwa na Umoja wa Falme za Kiarabu, Urusi imesema imetoa wanajeshi 150 wa Ukraine waliokuwa mateka kwa idadi sawa ya wanajeshi wa Urusi.
Wanajeshi wa Urusi walioachiliwa walipelekwa Belarus, mshirika wa Urusi, na wanapewa matibabu na kuwasiliana na familia zao, imesema wizara ya ulinzi ya Urusi ilisema.
Ukraine bado haijatoa tamko lolote. Vilevile Ukraine haichapishi idadi ya wafungwa wa kivita wanaoshikiliwa na Urusi, lakini inadhaniwa kuwa ni zaidi ya 8,000.
Urusi imepata mafanikio makubwa katika medani ya vita mwaka huu, jambo ambalo limezusha hofu huenda idadi ya wanajeshi wa Ukraine wanaokamatwa inaongezeka.
Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tedros Adhanom Ghebreyesus ametoa wito wa kukomeshwa mashambulizi dhidi ya hospitali za Gaza.
"Hospitali za Gaza kwa mara nyingine tena zimekuwa uwanja wa vita na mfumo wa afya uko katika tishio kubwa," amesema Dkt. Tedros.
Kauli yake imekuja baada ya hospitali ya mwisho iliyozingirwa kaskazini mwa Gaza, Kamal Adwan, kuvamiwa na na jeshi la Israel siku ya Ijumaa na hospitali mbili katika mji wa Gaza kushambuliwa siku ya Jumapili.
Jeshi la Israel limesema maeneo mawili kati ya hayo yalikuwa yakitumika kama vituo vya kamandi vya Hamas.
Dkt. Tedros pia amejiunga na makundi ya kutetea haki za binadamu kutaka kuachiliwa mara moja kwa mkurugenzi wa Kamal Adwan, Dkt. Hussam Abu Safiya, ambaye ameshikiliwa na vikosi vya Israel.
Jeshi la Israel lilisema siku ya Jumamosi kwamba hospitali yake ni "ngome" ya Hamas na wanajeshi wamewaua "magaidi" wapatao 20 na kuwaweka kizuizini wengine 240 wakati wa uvamizi huo.
Pia Jeshi hilo limesema Dkt. Abu Safiya ni miongoni mwa waliochukuliwa kuhojiwa na "anashukiwa kuwa gaidi wa Hamas."
Lakini Jeshi hilo halijatoa ushahidi wowote kuunga mkono madai hayo, ambayo Hamas imeyakanusha na kusema ni "uongo.”
Israel ilianzisha mashambulizi ya kuiangamiza Hamas kujibu mashambulizi ya kundi hilo kusini mwa Israel tarehe 7 Oktoba 2023, ambapo watu 1,200 waliuawa na wengine 251 walichukuliwa mateka.
Zaidi ya watu 45,540 wameuawa huko Gaza tangu mashambulizi huo, kulingana na wizara ya afya ya eneo hilo.
Pia unaweza kusoma:
Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF), imetupilia mbali malalamiko ya timu ya taifa ya Guinea dhidi ya Taifa Stars ya Tanzania, yaliyowasilishwa na Shirikisho la Mpira la Guinea kuhusu uhalali wa mchezaji wa Tanzania, Mohammed Ame.
Taarifa iliyotolewa cha Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), inaeleza kuwa, kwenye malalamiko hayo Guinea ilihoji uhalali wa mchezaji huyo kwa madai kuwa namba yake ya jezi aliyovaa, haikuwepo kwenye orodha ya wachezaji iliyowasilishwa kwa ajili ya mchezo huo.
Kutokana na uamuzi huo wa kamati ya nidhamu, matokeo ya mchezo huo mamba 143 yanabaki kama yalivyo na safari ya Tanzania kuelekea michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) inabaki pale pale.
Mchezo huo ulimalizika kwa Taifa Stars kuibuka na ushindi wa bao 1-0 mwezi Novemba, na kufuzu kwenye michuano ya AFCON, nchini Morocco, itakayofanyika Disemba mwakani.
Maafisa wanasema, takribani watu 71 wamekufa kusini mwa Ethiopia baada ya gari lao kutumbukia mtoni.
Gari hilo lililokuwa likisafiri katika jimbo la Sidama siku ya Jumapili, lilianguka mtoni wakati likipita darajani, afisa wa eneo hilo aliambia shirika la habari la Reuters.
Wosenyeleh Simion amesema abiria wengi walikuwa wakitoka kwenye sherehe ya harusi.
Polisi katika eneo hilo waliripoti kwamba gari hilo lilikuwa limejaa kupita kiasi, jambo ambalo huenda limechangia ajali hicho, iliyouwa wanaume 68 na wanawake 3.
Maelfu ya watu hufariki kila mwaka katika ajali za barabarani nchini Ethiopia, huku mwendo kasi na kutozingatia sheria za barabarani mara nyingi vikitajwa kuwa ndio chanzo.
Rais wa Azerbaijan, Ilham Aliyev ameitaka Urusi kukubali lawama kwa ajali ya ndege iliyotokea siku ya Krismasi na kuua watu 38 kati ya 67 waliokuwa ndani.
Ndege hiyo inaaminika ilishambuliwa na mifumo ya ulinzi ya anga ya Urusi ilipojaribu kutua Chechnya kabla ya kuelekezwa Kazakhstan, ambako ilianguka.
Siku ya Jumamosi, Rais wa Urusi Vladimir Putin alimwomba radhi rais wa Azerbaijan kwa kuanguka ndege hiyo katika anga ya Urusi - lakini hakukiri Urusi kuhusika.
Aliyev anaishutumu Moscow kwa kuficha kuhusika kwake katika ajali hiyo. Licha ya kukubali kuombwa radhi na Putin, amesema Urusi "lazima ikubali imehusika" na kulipa fidia.
Ndege hiyo ya shirika la ndege la Azerbaijan ilikuwa ikitoka Baku, mji mkuu wa Azerbaijan, kuelekea mji mkuu wa Chechnya wa Grozny tarehe 25 Disemba.
Pia unaweza kusoma:
Mtoto mchanga wa nne amekufa kutokana na baridi kali katika Ukanda wa Gaza, huku maelfu ya Wapalestina waliokimbia makazi yao ndani ya miezi 15 ya vita wakiwa katika mahema kando ya pwani yenye mvua na upepo wakati huu wa baridi.
Babake Jomaa al-Batran, anasema mwanawe mwenye umri wa siku 20, alifariki huku kichwa chake kikiwa cha "baridi kama barafu" mapema Jumapili.
Mtoto huyo alipelekwa katika katika Hospitali ya Al-Aqsa Martyrs akiwa mahututi.
Mtoto huyo ambaye ni pacha, walizaliwa mwezi mmoja kabla ya muda wao na walikaa siku moja tu katika chumba cha watoto katika hospitali hiyo, anasema Baba yao.
Kama vilivyo vituo vingine vya afya vya Gaza, hospitali hiyo imezidiwa na watu na inafanya kazi ya kutoa baadhi ya huduma tu.
Anasema madaktari walimwambia mama yao kuwaweka watoto hao wachanga katika joto, lakini haikuwezekana kwa sababu wanaishi kwenye hema na joto hushuka mara kwa mara chini ya nyuzi joto 10 nyakati za usiku.
"Tunaishi watu wanane, na tuna mablanketi manne tu," anasema al-Batran. Na kuongeza kuwa, “matone ya umande hupenya kwenye hema usiku kucha.”
Takribani watoto wengine watatu wamefariki kutokana na baridi kali katika siku za hivi karibuni, kwa mujibu wa mamlaka ya ndani ya afya ya Gaza.
Pia unaweza kusoma:
Mtalii mmoja amepoteza maisha na mwingine kujeruhiwa, baada ya kushambuliwa na papa katika ufuo wa Bahari Shamu nchini Misri, maafisa wanasema.
Katika taarifa ya wizara ya mazingira ya taifa hilo la kaskazini mwa Afrika, inasema tukio hilo lilitokea siku ya Jumapili kaskazini mwa mji wa Marsa Alam, mashariki mwa Misri, ambako ni eneo maarufu kwa wazamiaji.
Taarifa hiyo inaeleza tukio hilo lilitokea katika "maji yenye kina kirefu nje ya eneo lililotengwa la kuogelea."
Shirika la habari la AFP limeripoti kuwa watalii hao ni raia wa Italia, likinukuu chanzo ambacho hakikutajwa jina kutoka wizara ya mambo ya nje ya Italia.
Mwanaume mwenye umri wa miaka 48 aliyefariki alikuwa mkazi wa Roma, huku aliyejeruhiwa akiwa na umri wa miaka 69, kulingana na AFP.
Maafisa wa Misri wanasema watalii hao walisafirishwa hadi hospitali ya Port Ghalib, karibu maili 30 kaskazini mwa Marsa Alam.
Serikali inasema eneo la kuogelea huko Marsa Alam limefungwa na tukio hilo linachunguzwa.
Katika miaka 10 iliyopita, kumekuwa na vifo vinne vilivyothibitishwa kutokana na mashambulizi ya papa katika Bahari ya Shamu, kulingana na taarifa ya Taasisi huru ya Utafiti wa Papa.
Mara ya mwisho ilikuwa ni Juni 2023 karibu na mji wa Hurguda na lilihusisha mwanaume wa Urusi mwenye umri wa miaka 24.
Pia unaweza kusoma:
Mauaji ya kikatili ya mvulana huyo mwenye umri wa miaka 13 yalizua hasira kali miongoni mwa umma
Mahakama ya China imewahukumu wavulana wawili kwa kifo cha mwenzao mwezi Machi.
Vijana hao katika mkoa wa Hebei, waliotambuliwa tu kwa majina yao ya ukoo Zhang na Li, walikuwa na umri wa miaka 13 walipopanga njama ya kumuua mwenzao Wang na kugawana pesa zake.
Baada ya kumshambulia Wang kwa koleo, walimzika kwenye bustani ya mboga iliyoachwa, mahakama ilisema katika taarifa siku ya Jumatatu, na kuongeza kuwa "mbinu zao zilikuwa za kikatili na mbaya".
Vijana hao walihukumiwa kifungo cha maisha na kifungo cha miaka 12, mtawalia.
Wang alikuwa ameonewa kwa muda mrefu shuleni na wanafunzi wenzake watatu, familia yake na wakili walisema mwezi Machi, wakati mahakama Jumatatu ilibainisha kuwa alikuwa na mgogoro na Zhang na Li.
Winga wa Liverpool Mohamed Salah anasema "yuko mbali" kusaini mkataba mpya katika klabu hiyo ya Ligi ya Primia.
Salah, mwenye umri wa miaka 32, mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu na anaweza kuingia kwenye mazungumzo na klabu zisizo za Uingereza Januari 1 kuhusu uhamisho wa bila malipo mara tu mkataba wake utakapokamilika.
Mmisri huyo alifunga bao lake la 20 msimu huu lLiverpool ilipoilaza West Ham 5-0 kwenye wanja wa London Stadium Jumapili na kuendeleza uwepo wao kileleni mwa jedwali hadi pointi nane.
Alipoulizwa kuhusu mustakabali wake kufuatia ushindi huo, Salah aliiambia Sky Sports: "Hapana, tuko mbali na [mkataba] huo na sitaki kusema chochote kwenye vyombo vya habari.
Unaweza pia kusoma:
Familia zilizochanganyikiwa za waathiriwa zimekusanyika katika uwanja wa ndege huku wakisubiri miili ya wapendwa wao kutolewa, huku wengi wao wakipiga kambi usiku kucha.
Ajali ya ndege ya Korea Kusini, ilisababisha vifo vya watu 179, wakiwemo abiria na wahudumu wa ndege siku ya Jumapili.
wakati ndege hiyo aina ya Boeing 737-800 ilipotua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Muan. Wahudumu wawili wa ndege hiyo walinusurika na kupelekwa hospitalini.
Maafisa wameendelea kuchunguza vifusi baada ya ajali hiyo. Kaimu Rais Choi Sang-mok amewasili katika uwanja wa ndege leo asubuhi kukutana na familia za waathiriwa.
Serikali ya Korea Kusini imetangaza kipindi cha maombolezo cha kitaifa kwa siku saba zijazo.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu, makundi ya watetezi, vijana, na walionusurika katika utekaji nyara wa mwaka huu nchini Kenya wametangaza kuwa maandamano yaliyopangwa kufanyika siku ya Jumatatu nchini kote kupinga utekaji nyara unaoendelea na kupotea kwa watu unaotekelezwa yataendelea kama ilivyopangwa katika kaunti zote 47.
Wanasema kuwa maandamano hayo yanalenga kuishinikiza serikali kuwaachilia huru wale wanaoaminika kutekwa nyara, kukomesha kukamatwa kiholela kwa wanaotekwa, na pia kushughulikia madai yaliyotolewa na waandamanaji vijana wa Generation Z mwezi Juni.
Ongezeko la hivi majuzi la matukio ya utekaji nyara la zaidi ya watu 10 mwezi wa Disemba pekee na zaidi ya 80 kwa mwaka limezua ghadhabu kote nchini Kenya.
Licha ya serikali kukanusha, mashirika ya kutetea haki za binadamu, waathiriwa na wanaharakati wa vijana wanatoa wito kwa Wakenya kujiunga na maandamano ya kitaifa ya Jumatatu ya kutaka kuachiliwa kwa wale waliotekwa nyara na maafisa wa usalama na kukomesha kukamatwa kwa watu wanaoendelea.
Maandamano ya aina hii yamekuwa yakizuia na polisi kwa mabomu ya kutoa machozi na kukamatwa kwa baadhi ya waandamanaji.
Unaweza kusoma pia:
Pongezi zimekuwa zikimiminika kutoka kwa viongozi wa dunia kwa Jimmy Carter, ambaye aliwahi kuwa rais wa 39 wa Marekani kuanzia 1977 hadi 1981.
Unaweza pia kusoma:
Uchaguzi mpya nchini Syria unaweza kuchukua hadi miaka minne, kiongozi wa waasi Ahmed al-Sharaa amesema katika mahojiano ya matangazo.
Hii ni mara yake ya kwanza kutoa ratiba ya uchaguzi unaowezekana nchini Syria tangu kundi lake la Hayat Tahrir al-Sham (HTS) liongoze mashambulizi ya waasi yaliyomuondoa madarakani aliyekuwa Rais Bashar al-Assad.
Katika mahojiano na shirika la utangazaji la serikali ya Saudi Al Arabiya siku ya Jumapili, alisema kuandaa katiba mpya kunaweza kuchukua hadi miaka mitatu.
Alisema pia inaweza kuchukua mwaka mmoja kabla ya Wasyria kuanza kuona mabadiliko makubwa na maboresho ya huduma za umma kufuatia kupinduliwa kwa utawala wa Assad.
Sharaa alisema Syria inahitaji kujenga upya mfumo wake wa sheria na italazimika kufanya sensa kamili ya watu ili kuendesha uchaguzi halali.
Unaweza pia kusoma:
Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 100, kituo alichoanzisha kimethibitisha.
Mkulima huyo wa zamani wa karanga aliishi muda mrefu kuliko rais yeyote katika historia ambapo alisherehekea siku yake ya kuzaliwa ya 100 mnamo Oktoba.
Kituo cha Carter, ambacho kinatetea demokrasia na haki za binadamu kote duniani, kilisema alifariki Jumapili mchana nyumbani kwake huko Plains, Georgia.
Mwanademokrasia huyo alihudumu kama rais kuanzia mwaka 1977 hadi 1981, kipindi ambacho kilikumbwa na migogoro ya kiuchumi na kidiplomasia.
Baada ya kuondoka Ikulu ya White House na viwango vya chini vya idhini, sifa yake ilirejeshwa kupitia kazi ya kibinadamu ambayo ilimletea Tuzo ya Amani ya Nobel.
"Baba yangu alikuwa shujaa, sio kwangu tu bali kwa kila mtu anayeamini katika amani, haki za binadamu, na upendo usio na ubinafsi," mwanawe, Chip Carter, alisema katika taarifa.
"Dunia ni familia yetu kwa sababu ya jinsi alivyoleta watu pamoja, na tunakushukuru kwa kuheshimu kumbukumbu yake kwa kuendelea kuishi imani hizi za pamoja."
Carter - ambaye kabla ya kuwa rais alikuwa gavana wa Georgia, luteni katika jeshi la wanamaji la Marekani na mkulima - ameacha watoto wake wanne, wajukuu 11 na vitukuu 14.
Mkewe, Rosalynn, ambaye alikuwa walioana miaka 77, alikufa mnamo Novemba 2023.
Unaweza pia kusoma: