Israel yashambulia malengo 200 ya Hezbollah nchini Lebanon katika muda wa saa 24
Huku mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Marekani na Iran yakiendelea mjini Islamabad, Pakistan, Israel inasema inaendelea na mashambulizi chini Lebanon.
Jeshi la Israel (IDF) linasema kuwa limeshambulia zaidi ya shabaha 200 za Hezbollah nchini Lebanon katika muda wa saa 24 zilizopita.
Katika taarifa, Isarel inasema jeshi lake la anga linafanya mashambulizi zaidi na kusaidia vikosi vya ardhini vinavyofanya kazi kusini mwa Lebanon.
IDF pia inasema inalenga kuzuia mashambulizi dhidi ya Israel. Wizara ya afya ya Lebanon imesema watu sita wameuawa katika uvamizi kusini mwa Lebanon, huku wengine watano wakijeruhiwa.
Wakati huo huo, Israel imeonya kuhusu uvamizi wa ndege katika eneo la Upper Galilee kaskazini mwa nchi hiyo.
Haijabainika ni nani aliyeanzisha shambulio hilo.
Maelezo zaidi: