Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Moja kwa moja, Marekani kudhibiti kijeshi bandari za Iran kuanzia leo, Trump akisema 'hajali' ikiwa Tehran itarejea kwenye mazungumzo

Iran inasema ''haitababaishwa na vitisho vya Marekani'' ikiongeza kuwa mazingumzo ya Islamabad yalifeli kutokana na ''Washington kubadili misimamo''.

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Ambia Hirsi

  1. Iran bado inataka silaha ya nyuklia, Trump anasema

    Rais wa Marekani anasema Iran bado inataka kuwa silaha ya nyuklia na alieleza nia hiyo wakati wa mkutano mjini Islamabad. "

    Bado wanataka kuwa na sila haio, na waliliweka wazi hilo usiku uliopita. Iran kamwe haitakuwa na silaha ya nyuklia."

    Trump tayari amesema mazungumzo ya moja kwa moja na Iran yalitibuka kwa sababu Tehran "haikuwa tayari kuachana na malengo yake ya nyuklia".

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi hapo awali alisema pande hizo mbili ziko "zinakaribia" kufikia makubaliano lakini Iran ilikabiliwa na " visa vya kubadilisha misimama hapa na pale".

    Soma zaidi:

  2. Péter Magyar ashinda uchaguzi wa Hungary kwa kishindo

    Peter Magyar ameshinda uchaguzi mkuu wa Hungary,huku chama chake kikipata theluthi mbili ya viti vya ubunge katika uchaguzi ambao unamuondoa madarakani Waziri Mkuu Victor Orban aliyeliongoza taifa hilo kwa miaka 16.

    Bwana Magyar ameuambia umati mkubwa wa wafuasi mjini Budapest kuwa Hungary inataka tena kuwa taifa la Ulaya na kuongeza kuwa wamefanikiwa kuleta muujiza katika historia ya Hungary kwa kushinda uchaguzi huo kwa kishindo.

    Waziri Mkuu huyo ajaye wa Hungary ameahidi kipindi cha kukabidhiana madaraka kitakuwa cha amani.Viongozi kadhaa wa nchi za Umoja wa Ulaya wamempongeza Magyar kwa ushindi huo.

  3. Trump amshambulia Papa Leo juu ya Iran

    Donald Trump amemkosoa vikali Papa Leo XIV kwenye mitandao ya kijamii baada ya kiongozi wa kwanza wa Marekani wa Kanisa Katoliki Duniani kulaani tishio la rais wa Marekani dhidi ya Iran.

    Katika chapisho refu kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, rais huyo wa Marekani aliandi Papa "ni mbaya kwa Sera ya Kigeni".

    "Simtaki Papa ambaye anadhani ni sawa kwa Iran kuwa na Silaha ya Nyuklia," Trump alisema.

    Akiorodhesha malalamiko mengine dhidi ya Papa, Trump aliandika kwamba Papa Leo ni "Weak on Crime, Weak on Nuclear Weapons".

    Wiki iliyopita, Papa Leo alikosoa tishio la Trump kwamba "ataiangamiza Iran usiku wa leo" nchi hiyo isipofikia makubaliano ya kumaliza vita.

    Akisisitiza kuwa tamko kama hilo "halikubaliki", Papa aliongeza kusema: "Kuna maswali ya sheria ya kimataifa, lakini zaidi ya yote, ni suala la kimaadili."

  4. Marekani kudhibiti kijeshi bandari za Iran kuanzia leo

    Jeshi la Marekani linasema litaanza kuzingira bandari za Iran siku ya Jumatatu, lakini "haitazuia" meli zinazopita kwenye Mlango wa bahari wa Hormuz zinazosafiri kwenda au kutoka nchi nyingine.

    Haya ndio matukio ya hivi punde kwa ufupi:

    • Kamandi Kuu ya Marekani imesema kuwa itaanza kuiza meli zinazoingia na kutoka katika bandari za Iran saa 10:00 ET (14:00 GMT) siku ya Jumatatu.
    • Rais wa Marekani Donald Trump anasema agizo lake ni la kujibu hayua ya Iran "kukataa makusudi" kufungua tena Mlango wa bahari wa Hormuz. Pia anaonya Jeshi la Wanamaji la Marekani "litawaangamiza Wairani wowote watakaowashambulia na watazuia meli yoyote itakayolipa ushuru wa usafiri kwenda Iran.
    • Bei ya Mafuta ghafi imeongezeka tena na kupindukia dola mia moja baada ya mazungumzo kati ya Marekani na Iran kufeli kufikia makubaliano kuvimaliza vita vya Mashariki ya Kati. Bei ya Mafuta imekuwa ikipanda na kushuka tangu vita vya Iran kuzuka mwishoni mwa mwezi Februari na shughuli za usafiriki kuathirika katika Mlango Bahari wa Hormuz ambapo asilimia 20 ya Mafuta na gesi hupitia.
    • Trump anasema mazungumzo ya moja kwa moja na Iran mjini Islamabad yalifeli kwa sababu "Iran haiko tayari kuachana na malengo yake ya nyuklia"
    • Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi anasema Tehran ilishiriki mazungumzo hayo kwa "imani njema" huku spika wa bunge la Iran, Mohammad Bagher Ghalibaf, Spika akiongeza kuwa nchi yake haitatishika baada ya Rais Donald Trump kusema Jeshi la Majini la Marekani litaanza mara moja operesheni ya kuzuia Meli kupita Katika Mlango Bahari wa Hormuz

    Pia unaweza kusoma:

  5. Karibu kwa Matangazo ya Moja kwa mojaleo Jumatatu 13.04.2026