Moja kwa moja, Iran yatishia kulipiza kisasi iwapo meli zake za mafuta zitashambuliwa

Jeshi la Iran (IRGC) limetishia kulenga maeneo ya Marekani iwapo meli za mafuta za Iran zitashambuliwa, huku Washington ikiwa bado inasubiri majibu ya Tehran kuhusu pendekezo lake la hivi karibuni la mazungumzo.

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Beldeen Waliaula

  1. India yafanyia majaribio kombora jipya lenye uwezo wa kurusha makombora mengi kwa wakati mmoja

    .

    Chanzo cha picha, Hindustan Times via Getty

    Jeshi la India limefanyia majaribio kizazi kipya cha makombora ya hali ya juu ya Agni kwenye pwani ya Odisha.

    Kombora hili linaweza kurusha makombora mengi katika maeneo tofauti.

    Kulingana na Wizara ya Ulinzi ya India, mfumo huu wa makombora ulijaribiwa mnamo Ijumaa, Mei 8.

    "India mnamo Mei 8 ilifanikiwa kujaribu kombora la hali ya juu la Agni lenye mfumo wa MIRV kutoka Kisiwa cha Abdul Kalam, Odisha," Wizara ya Ulinzi ilisema katika taarifa.

    Taarifa hiyo iliendelea kwa kusema kuwa kombora hilo lenye vichwa vingi vya kivita, lililenga maeneo kadhaa yaliyotengwa katika eneo pana la kijiografia katika Bahari ya Hindi.

    Uzalishaji wa makombora ya Agni ulianza nchini India mwaka 1983. Kizazi kilichopita (cha tano) Agni ni balestiki nunayoweza kusafiri kutoka bara moja hadi jingine pamoja na kuwa na uwezo wa kubeba kichwa cha nyuklia, mbali na kwamba kombora hilo linaweza kusafiri umbali wa kilomita 5,000.

  2. Jeshi la Israel latangaza kuwaua zaidi ya wapiganaji 10 wa Hezbollah

    Uharibifu ulioshuhudiwa baada ya shambulizi la Israel nchini Lebanon

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Uharibifu ulioshuhudiwa baada ya shambulizi la Israel nchini Lebanon

    Wizara ya Afya nchini Lebanon imetangaza kuwa idadi ya vifo inayotokana na mashambulizi ya Israel yaliyofanyika hapo jan imefikia watu 39.

    Kulingana na wizara hiyo moja ya mashambulizi ya Israel katika mji wa Saskia kusini mwa Lebanon ilisababisha vifo vya watu saba, akiwemo mtoto mmoja.

    Jeshi la Israel lilisema mashambulizi hayo yalilenga wapiganaji wa Hezbollah, na kuongezea kuwa “linafahamu kuhusu vifo vya raia.”

    Tangu Rais wa Marekani Donald Trump kutangaza makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya serikali ya Israel na Lebanon mwezi Aprili tarehe 16, mashambulizi na mapigano kati ya jeshi la Israel na Hezbollah bado yanaendelea.

    Jeshi la Israel lilisema hii leo kuwa vikosi vyake vimewaua zaidi ya wapiganaji 10 wa Hezbollah na kushambulia takriban maeneo 40 na kuharibu miundombinu ya kundi hilo katika saa 24 zilizopita.

    Pia unaweza kusoma:

  3. Putin asema vita vya Urusi na Ukraine viko karibu kumalizika

    Picha ya Vladimir Putin

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Picha ya Vladimir Putin

    Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kuwa anaamini vita vya Ukraine vinaeleka kufika tamati,alitoa kauli hiyo saa chache tu baada ya kusema atashinda vita nchini Ukraine wakati wa gwaride la Siku ya Ushindi mjini Moscow.

    “Nadhani suala hili linaelekea kuisha,” Putin aliwaambia waandishi wa habari kuhusu vita vya Urusi na Ukraine, ambavyo ni vita vibaya kuwahi kushuhudiwa bara Ulaya tangu Vita vya Pili vya Dunia.

    Aidha Putin aliongezea kuwa yuko tayari kujadili mipango mipya ya usalama bara Ulaya, na kupendekeza kuwa mshirika wake katika mazungumzo hayo atakuwa Kansela wa zamani wa Ujerumani Gerhard Schröder.

    Pia unaweza kusoma:

  4. Meli ya watalii iliyokumbwa na mlipuko wa virusi vya Hantavirus yawasili Tenerife

    Meli katika bandari ya Granadilla
    Maelezo ya picha, Meli katika bandari ya Granadilla

    Takriban mwezi mmoja baada ya abiria wa kwanza kufariki kutokana na virusi vya hantavirus akiwa ndani ya meli ya watalii ya MV Hondius, meli hiyo imewasili Tenerife katika Visiwa vya Canary.

    Maandalizi makubwa yamekuwa yakiendelea ili kuipokea meli hiyo katika bandari ya Granadilla na kusaidia zaidi ya watu 100 kurejeshwa makwao.

    Meli ya Hondius haijaruhusiwa kufika bandarini, lakini imesalia eneo salama baharini karibu na kisiwa hicho, ili iendelee kubaki katika hali ya kutengwa ili kuzuia maambukizi kwa wananchi wa kawaida wa Hispania.

    Pia unaweza kusoma:

  5. Iran yaonya kushambulia vituo vya kijeshi vya Marekani na meli za adui iwapo meli zao mafuta zitalengwa

    Picha ya meli

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Picha ya meli

    Jeshi la Iran (IRGC) limetishia kulenga maeneo ya Marekani iwapo meli za mafuta za Iran zitashambuliwa, huku Washington ikiwa bado inasubiri majibu ya Tehran kuhusu pendekezo lake la hivi karibuni la mazungumzo.

    Katika taarifa iliyotolewa hapo jana, siku moja tu baada ya Marekani kushambulia meli mbili za mafuta za Iran katika Ghuba ya Oman, Iran imesema kwamba “shambulio lolote dhidi ya meli za mafuta na meli za kibiashara za Iran, zitawafanya washambulie vituo vya kijeshi vya Marekani Pamoja na meli za adui"

    Pia unaweza kusoma:

  6. Hujambo na karibu katika matangazo yetu ya moja kwa moja.