Vita vya Israel na Gaza: Kuna matumaini ya kufikia makubaliano ya kusitisha vita kwa muda
Ujumbe wa Hamas umeripotiwa kuwasili mjini Cairo, Misri, na kuongeza matumaini ya kusitishwa kwa mapigano katika vita vya Israel na Gaza.
Moja kwa moja
Ufaransa nchi ya kwanza kuweka haki ya utoaji mimba katika katiba
Chanzo cha picha, AFP
Ufaransa inajiandaa kuwa nchi ya kwanza duniani kuweka haki ya utoaji mimba katika katiba yake.
Siku ya Jumatatu, wabunge kutoka mabaraza ya juu na ya chini watakutana katika kikao maalumu katika Ikulu ya Versailles, kilichoitishwa na Rais Emmanuel Macron.
Ikiwa, kama inavyotarajiwa, watapigia kura hoja ya serikali kwa kura tatu kwa tano, basi katiba ya nchi ya 1958 itarekebishwa ili kuweka "uhuru uliohakikishwa" wa wanawake wa kutoa mimba.
Itakuwa marekebisho ya 25 kwa hati ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya Tano, na ya kwanza tangu 2008.
Wafuasi wanashangilia kuhusu marekebisho hayo ambayo wanaona kama bima dhidi ya unyanyapaa kama huo nchini Ufaransa.
Kura za maoni zinaonesha karibu 85% ya umma wa Ufaransa wanaunga mkono mageuzi hayo.
Upinzani kutoka kwa watetezi wa mrengo wa kulia bungeni umeshindwa kutekelezwa.
Vita vya Ukraine: Urusi yasema ilizuia ndege 38 za Ukraine zisizo na rubani zinazoshambulia Crimea
Chanzo cha picha, Reuters
Milipuko mfululizo imetikisa Crimea, baada ya kuripotiwa shambulio la ndege zisizo na rubani za Ukraine kwenye peninsula ambayo ilitwaliwa na Urusi mwaka 2014.
Video iliyowekwa mtandaoni inaonyesha mlipuko unaodaiwa kuwa karibu na ghala la mafuta katika mji wa kusini-mashariki wa Feodosiya. Maafisa wa Urusi walisema ndege zisizo na rubani 38 zilidunguliwa.
Daraja la Kerch linalounganisha Crimea na Urusi lilifungwa kwa muda.
Shambulio hilo limetokea huku Ukraine ikiendelea kuwahimiza washirika kuongeza usambazaji wa silaha.
Wanajeshi wa Urusi hivi karibuni wamepata mafanikio nchini Ukraine huku Kyiv ikijitahidi kudumisha vikosi vyake kwa silaha zinazotengenezwa na nchi za Magharibi.
Moscow ilichukua udhibiti mwezi uliopita wa mji muhimu wa mashariki wa Avdiivka.
Urusi haijaripoti uharibifu wowote kutoka kwa shambulio la hivi punde huko Crimea, ingawa walioshuhudia wameripoti kutikisika kwa madirisha na honi za gari kulia.
Kyiv haijathibitisha kuhusika kwa vikosi vyake.
Siku ya Jumamosi, ndege isiyo na rubani ya Urusi iligonga jengo la ghorofa katika mji wa Odesa nchini Ukraine, na kuua takribani watu 10, akiwemo mtoto mchanga wa miezi minne.
Siku ya Jumapili, Urusi ililenga eneo la kusini la Kherson, na kuua mtu mmoja na kuwajeruhi wengine watatu, kwa mujibu wa maafisa wa Ukraine.
Vita vya Israel na Gaza: Kuna matumaini ya kufikia makubaliano ya kusitisha vita kwa muda
Chanzo cha picha, EPA
Ujumbe wa Hamas umeripotiwa kuwasili mjini Cairo, Misri, na kuongeza matumaini ya kusitishwa kwa mapigano katika vita vya Israel na Gaza.
Afisa mmoja wa Marekani ambaye jina lake halikutajwa amesema Israel "kwa kiasi fulani" mpango huo.
Marekani inasema mapumziko hayo ya wiki sita yatashuhudia kuachiliwa kwa mateka zaidi wa Israel na wafungwa wa Kipalestina.
Shinikizo la makubaliano hayo liliongezeka baada ya tukio la Alhamisi nje ya Mji wa Gaza kaskazini mwa eneo hilo ambapo takribani watu 112 waliuawa wakati umati wa watu ulipokuwa ukikimbilia msafara wa misaada.
Hamas imeishutumu Israel kwa kuwafyatulia risasi raia walipokuwa wakijaribu kupata chakula.
Israel imekanusha hili, na Jumapili ilisema mapitio ya awali yalihitimisha kwamba wanajeshi wa Israeli walipiga risasi "watu kadhaa" ambao waliwakaribia, lakini kwamba vifo vingi vilisababishwa na mkanyagano wa watu.
Maafisa wa Misri, ambao wamekuwa wakiongoza mazungumzo na Qatar, walisema wajumbe kutoka Hamas na Israel wanatarajiwa kuhudhuria mazungumzo hayo.
Hamas inaripotiwa kusema kwamba makubaliano kuhusu usitishaji vita yanaweza kufikiwa ndani ya saa 24 hadi 48 zijazo, huku chanzo kutoka kundi hilo kikiambia vyombo vya habari vya Misri makubaliano yanayotegemea Israel kukubaliana na matakwa yake.
Matarajio ya makubaliano hayo yalitolewa baada ya afisa mkuu wa Marekani kusema Israel kwa upande wake "imekubali kimsingi" mfumo wa kusitisha mapigano kwa wiki sita.
Jeshi la Israel lilianzisha kampeni kubwa ya anga na ardhini kuiangamiza Hamas baada ya watu wenye silaha kuwaua takribani watu 1,200 kusini mwa Israel tarehe 7 Oktoba na kuwarudisha 253 huko Gaza kama mateka.
Wizara ya afya ya Gaza inayoendeshwa na Hamas imesema takribani watu 30,410 wakiwemo watoto na wanawake 21,000 wameuawa huko Gaza tangu wakati huo huku wengine 7,000 wakitoweka na 71,700 kujeruhiwa.
Fahamu chanzo cha kifo cha msanii maarufu wa Nigeria 'Mr. Ibu'
Chanzo cha picha, REALMRIBU/INSTAGRAM
Mchekeshaji maarufu wa Nigeria, John Okafor almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia siku ya Jumamosi baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Bw. Ibu alifariki akiwa katika hospitali moja mjini Lagos alipokuwa akipatiwa matibabu.
Rais wa Chama cha Waigizaji wa Filamu wa Nigeria, Emeka Rollas alithibitisha taarifa za kifo cha Bw. Ibu siku ya Jumamosi.
Alieleza kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa:
“Ni kwa masikitiko makubwa nawatangazia kuwa bwana Ibu amefariki dunia. baada ya kusumbuliwa na tatizo la moyo kwa miaka 24.
Jinsi bwana Ibu alivyohangaika na matibabu
Mnamo Oktoba 2023, video ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ambapo kuna mvulana alionekana akiwauliza wapendwa wake wamjumuishe katika maombi.
Katika video hiyo, Bw. Ibu alisema kuwa amekaa kwa muda mrefu hospitalini kwa sababu ya ugonjwa "usiotibika.
Katika video hiyo, alisema kuwa madaktari walipendekeza kukatwa miguu yake.
Aliongeza kuwa “Kwa sasa bado naendelea na matibabu hospitalini, Mkuu wa hospitali hiyo alisema bora nikatwe mguu ikiwa wanachokwenda kukifanya hakitafanikiwa.
Kisha akawaomba wapendwa wake wamwombee ili asikatwe mguu wake.
Historia ya Bwana Ibu
John Okafor
Mr.Ibu ni muigizaji na mchekeshaji ambaye alitokea Dabe katika jimbo la Enugu kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Ameonekana katika mamia ya sinema za Nollywood ndani na nje ya Nigeria.
Alipata umaarufu kwa jinsi alivyoweza kudhibiti uso wake anapotaka kuwachekesha watazamaji.
Kwa nyakati tofauti, alikuwa akicheza muziki na kucheka ili kuburudisha hadhira.
Mnamo Disemba 2023, familia ya Bw. Ibu ilieleza ugonjwa wake wakati ambapo habari zilisambaa mtandaoni kuwa miguu yote miwili ya bwana Ibu imekatwa.
Hata hivyo, mmoja wa wanafamilia yake aitwaye Valentine Okafor alisema kwenye ukurasa wake wa Instagram kwamba mguu wa Bw. Ibu ulikatwa.
Familia hiyo pia ilieleza ukweli kuhusu ugonjwa wake, ikisema kuwa yeye haugui kisukari, lakini “mara nyingi anatokwa na damu miguuni (kuharibika kwa mishipa ya damu)” na magonjwa mengine yanayotishia maisha yake.
Meli inayomilikiwa na Uingereza, iliyoshambuliwa na waasi wa Houthi yazama katika pwani ya Yemen
Meli ya mizigo iliyosajiliwa na Uingereza imezama wiki mbili baada ya kushambuliwa na Wahouthi katika Ghuba ya Aden.
Serikali ya Yemen ilisema meli ya Rubymar ilikuwa ikiteleza na kuingia maji kwa siku kadhaa kabla ya kuzama.
Ni meli ya kwanza kuzamishwa na waasi wanaoungwa mkono na Iran nchini Yemen tangu waanze kulenga meli katika Bahari ya Shamu.
Meli hiyo iliripotiwa kubeba mbolea na wataalamu wanasema kuzama kunahatarisha "janga la kimazingira".
Rubymar ilikuwa katika Ghuba ya Aden karibu na Mlango-Bahari wa Bab al-Mandab ilipopigwa na makombora mawili yaliyorushwa na waasi wa Houthi wenye makao yake Yemen.
BBC ilipata picha ya meli hiyo tarehe 21 Februari, ambayo ilionesha ikiwa imezama, lakini bado ilikuwa ikielea.
Meli hiyo iliaminika kuwa imebeba shehena ya mbolea ya ammonium nitrate. Waziri Mkuu wa serikali ya Yemen inayotambulika kimataifa, Ahmed Awad Bin Mubarak, aliitaja kuzama kwa meli hiyo "ni janga la kimazingira ambalo halijawahi kutokea".
Greenpeace ilisema kumwagika kwa nitrati ya ammoniamu kunaweza kuwa na "athari kubwa kwa mifumo ikolojia ya baharini", ambayo kusini mwa Bahari ya Shamu ina miamba ya matumbawe, mikoko ya pwani na viumbe mbalimbali vya baharini.
Idara ya Sayansi ya Bahari katika Chuo Kikuu cha Jordan ilisema kuwa kutolewa kwa kiasi kikubwa cha mbolea baharini kunaweza kuchochea ukuaji wa ziada wa mwani, kwa kutumia oksijeni nyingi na kwamba viumbe vya kawaida vya baharini haviwezi kuishi.
Watu wa Gaza watoa maelfu ya dola ili kukwepa mashambulizi
Chanzo cha picha, Getty Images
Huku mashambulizi mabaya ya Israel yakishambulia na uhaba mkubwa wa chakula ukiendelea, na operesheni hatari ya kijeshi ya Israel kusini mwa Gaza ikikaribia, Wapalestina zaidi na zaidi wanatafuta njia ya kutoka, ikiwa wanaweza kupata pesa kwa ajili hiyo.
Kuondoka huku kwa uhakika kunahitaji watu walipe maelfu ya dola na ili kuingiza majina yao kwenye orodha ya watu walioidhinishwa kuondoka kupitia kivuko cha Rafah kwenda Misri.
Kivuko hicho kimefungwa kwa idadi kubwa ya watu chini ya kizuizi cha Misri na Israeli dhidi ya Hamas.
Ni baadhi tu ya wamiliki wa pasipoti za kigeni na wategemezi wao wameweza kuondoka, pamoja na baadhi ya watu waliojeruhiwa vibaya na wagonjwa na wale wanaoandamana nao.
Hata hivyo, kuna mfumo sambamba ambapo wananchi wa Gaza wanalipa madalali wa Misri kuingia kwenye orodha ya watu wanaoweza kuondoka.
Bei inaelezwa kuwa huanzia $6,000 (£4,800) kwa kila mtu hadi zaidi ya $12,000, kiasi kikubwa mno kwa wakazi wengi wa Gaza.
Bado idadi inayoongezeka ya watu wanajaribu kutafuta pesa ili kukimbia, kwa msaada wa marafiki na familia huko Amerika na Ulaya.
Marekani yapeleka msaada wa kwanza wa kibinadamu huko Gaza
Marekani imetekeleza ombi la msaada wa kwanza kibinadamu kwa Gaza, huku zaidi ya milo 30,000
ikiingizwa kwa parachuti na ndege tatu za kijeshi.
Operesheni hiyo iliyotekelezwa kwa pamoja na jeshi la anga
la Jordan, ilikuwa ya kwanza kati ya nyingi zilizotangazwa na Rais Joe Biden.
Aliahidi kuongeza msaada baada ya takribani watu 112 kuuawa wakati
umati wa watu ukikimbilia msafara siku ya Alhamisi.
Hayo yanajiri huku afisa wa ngazi ya juu wa Marekani akisema
mpango wa makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda wa wiki sita huko Gaza
upo.
Afisa wa utawala wa Biden alisema Jumamosi kwamba Israeli
"imekubali zaidi au kidogo" makubaliano juu ya usitishaji mpya wa
mapigano.
"Itakuwa usitishaji vita wa wiki sita huko Gaza kuanzia
leo ikiwa Hamas itakubali kuachilia kundi lililobainishwa la mateka walio
hatarini, wagonjwa, waliojeruhiwa, wazee na wanawake," alisema afisa huyo
ambaye hakutajwa jina.
Siku ya Jumamosi ndege za C-130 zilidondosha zaidi ya milo
38,000 kwenye ufuo wa eneo hilo, Kamandi Kuu ya Marekani ilisema katika
taarifa.
"Hii ni sehemu ya juhudi endelevu za kupata misaada
zaidi katika Gaza, ikiwa ni pamoja na kupanua mtiririko wa misaada kupitia njia
za ardhini," iliongeza.
Nchi nyingine ikiwa ni pamoja na Uingereza, Ufaransa, Misri
na Jordan hapo awali zilipeleka misaada katika Gaza, lakini hii ni ya kwanza
kwa Marekani.
Maafisa wa utawala walisema kwamba "tukio la
kusikitisha" la Alhamisi limeangazia "umuhimu wa kupanua na kudumisha
mtiririko wa misaada ya kibinadamu katika Gaza ili kukabiliana na hali mbaya ya
kibinadamu".