Afisa wa jeshi la Israel akiri 'uharibifu mkubwa' katika kambi ya wakimbizi Gaza

Jeshi la Israel linasema "linajutia madhara yaliyowakumba raia wasio na hatia" katika kambi ya wakimbizi ya Maghazi.

Moja kwa moja

Lizzy Masinga and Ambia Hirsi

  1. Na kufikia hapo tunakamilisha matangazo haya ya moja kwa moja. Hadi kesho kwaheri.

  2. Mbongeni Ngema: Nguli wa sanaa wa Afrika Kusini aombolezwa

    Kazi za Mbongeni Ngema zilionyesha "roho ya upinzani" dhidi ya utawala wa wazungu wachache, familia yake ilisema.

    Chanzo cha picha, GALLO IMAGES

    Maelezo ya picha, GALLO IMAGES

    Salamu za rambirambi zimeendelea kutolewa kufuatia kifo cha mtunzi wa maigizo wa Afrika Kusini Mbongeni Ngema aliyefariki katika ajali ya gari akiwa na umri wa miaka 68.

    Alipata umaarufu wa kimataifa katika miaka ya 1980 kwa tamthilia zilizosawiri maisha ya watu weusi chini ya mfumo wa ubaguzi wa rangi wa ubaguzi wa rangi.

    Kazi zake "zilionyesha roho ya upinzani" wakati wa utawala wa wazungu wachache, familia yake ilisema

    Ngema alijulikana zaidi kwa muziki wake Sarafina!, ambao baadaye ulibadilishwa kuwa filamu iliyoigizwa na Whoopi Goldberg.

    Rais Cyril Ramaphosa aliongoza taifa kumuomboleza mtunzi wa maigizo na mwelekezajii wa tamthilia

    "Masimulizi ya ustadi wa Ngema ya mapambano yetu ya ukombozi yaliheshimu ubinadamu wa Waafrika Kusini waliokandamizwa" na "kufichua unyama" wa utawala wa kibaguzi, kiongozi huyo wa Afrika Kusini alisema.

    Alifariki katika ajali ya barabarani Jumatano jioni alipokuwa akirejea kutoka mazishini katika mji wa Lusikisiki lililopo jimbo la Eastern Cape.

    Zaidi ya watu 700 wamefariki katika ajali za barabarani nchini Afrika Kusini tangu mwanzoni mwa mwezi Disemba.

  3. Afisa wa IDF akiri 'uharibifu mkubwa' katika shambulio dhidi ya kambi za wakimbizi

    vv

    Chanzo cha picha, Ashraf Amra/Anadolu via Getty Images

    Afisa wa kijeshi wa Israel amesema kuwa matumizi ya mabomu yalisababisha "uharibifu mkubwa" katika mashambulizi yaliyolenga kambi ya wakimbizi ya Maghazi tarehe 24 Disemba.

    Kulingana na wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas, watu 70 waliuawa katika mashambulizi ya anga ya Israel dhidi ya hiyo siku ya Jumapili, huku idadi hiyo ikitarajiwa kuongezeka.

    Akizungumza na shirika la utangazaji la umma la Kan news, afisa mmoja wa kijeshi wa Israel alisema: "Aina ya silaha haikulingana na shambulio hilo, na imesababisha uharibifu mkubwa ambao ungeweza kuepukwa."

    Alisema tukio hilo linachunguzwa zaidi.

    Keshi la Ulinzi wa Israel IDF iliiambia BBC kwamba "inajutia madhara ya shambulizi hilo kwa watu wasio na hatia, na inajitahidi kupata funzo kutokana na tukio hilo".

    Jeshi lilisema ndege zake zilishambulia shabaha mbili karibu na eneo ambalo wanamgambo wa Hamas walikuwa lakini majengo yaliyokuwa karibu pia yaligongwa wakati wa shambulio hilo.

  4. Waziri Mkuu wa Ethiopia akutana na Kamanda wa Kikosi Maalum cha Sudan

    xx

    Chanzo cha picha, ABIY AHMED/TWITTER

    Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, amekutana na Kamanda wa Kikosi Maalum cha Sudan (RSF), Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo, mjini Addis Ababa

    Wawili hao wamekutana huku mazungumzo ya majenerali hao wawili wa Sudan na mazungumzo yao ya kwanza ya ana kwa ana yakiahirishwa.

    Waziri Mkuu Abiy hakutoa maelezo lakini alifanya mazungumzo na kamanda wa kijeshi anayejulikana kwa jina la Hemetis.

    Kabla ya kuondoka kwenda Addis Ababa, Hemet alisafiri hadi Uganda na kufanya mazungumzo na Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni.

    amanda wa Kikosi Maalum cha Sudan amekuwa akipigana na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan kwa miezi minane kuhusu mustakabali wa nchi hiyo.

    Mazungumzo ya kutafuta suluhisho la mzozo kati ya majenerali wawili wa Sudan yalipangwa kufanyika nchini Djibouti siku ya Alhamisi lakini yameahirishwa hadi mwezi ujao kutokana na "matatizo ya kiufundi".

    Tarehe ya mazungumzo nchini Djibouti bado haijaamuliwa.

    Juhudi za hapo awali za kutatua mzozo huo kwa amani ziligonga mwamba.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  5. Ndege ya abiria ya Urusi yatua kimakosa kwenye mto ulioganda

    Ndege hiyo ya abiria ilitua salama mtoni licha ya hitilafu ya rubani

    Chanzo cha picha, EAST SIBERIAN TRANSPORT PROSECUTOR'S OFFICE

    Maelezo ya picha, Ndege hiyo ya abiria ilitua salama mtoni licha ya hitilafu ya rubani

    Ndege ya abiria iliyokuwa na watu 34 imetua kwenye mto ulioganda katika eneo la Mashariki ya Mbali nchini Urusi, kwa sababu ya makosa ya rubani.

    Hakuna aliyeumia wakati ndege ya shirika la ndege la Polar Airlines ya zama za Soviet Antonov An-24 iliposimama Alhamisi asubuhi karibu na nchi kavu, kwenye Mto Kolyma ulioganda.

    Ndege hiyo ilitua kwenye barabara ya uwanja wa ndege wa Zyryanka.

    Maswali ya awali yalisema makosa ya majaribio ndiyo ya kulaumiwa, waendesha mashitaka walisema.

    Abiria thelathini na wafanyakazi wanne walikuwa ndani ya ndege hiyo.

    Ndege ya PI217 iliondoka Yakutsk, mji mkuu wa jamhuri ya Sakha Mashariki ya Mbali ya Urusi, mapema Alhamisi.

    Ilikuwa inaelekea Zyryanka, kilomita 1,100 kaskazini-mashariki, na ilitakiwa kwenda hadi mji wa Srednekolymsk kabla ya kurejea Yakutsk.

    Video kutoka kwa mmoja wa abiria ilionyesha ndege hiyo karibu katikati ya Mto Kolyma ulioganda mashariki mwa Siberia.

    Kiwango cha joto mjini Zyryanka hushuka hadi karibu 40C wakati huu wa mwaka.

    Waendesha mashtaka walisema ndege hiyo ilikuwa imetua kwenye ukingo wa mchanga kwenye mto huo.

    XX

    Chanzo cha picha, EAST SIBERIAN TRANSPORT PROSECUTOR'S OFFICE

  6. Watu 40 wafariki katika maporomoko ya udongo DR Congo

    Watu 40 wamethibitishwa kutokana na maporomoko ya udongo na mafuriko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kufuatia mvua kubwa iliyonyesha Jumanne.

    Wakazi wamekuwa wakichimba matope kutafuta maiti. Baadhi ya watu wamesombwa na maji ya mafuriko.

    Takriban watu 20 walikufa Bukavu, na wengine 20 pia waliuawa katika kijiji cha Burinyi, kilomita 50 kutoka Bukavu.

    Mamlaka ya mkoa imesema kuwa inatathmini hali hiyo ili kutoa usaidizi unaohitajika kwa jamii zilizoathirika.

    Siku ya Jumanne, tukio sawia na hilo lilitokea Kasai, jimbo la kati, na kusababisha vifo vya watu 20 na kuharibu miundombinu mingi.

    Mafuriko na maporomoko ya udongo hutokea mara kwa mara nchini DRC na mara nyingi yanakuwa mabaya zaidi kutokana na msongamano wa watu mijini na miundombinu dhaifu, ambayo imefanya jamii kuwa hatarini zaidi.

    Kulingana na Umoja wa Mataifa, mabadiliko ya hali ya hewa yamesababisha mvua kubwa katika baadhi ya sehemu za bara Afrika, na matokeo yake ni mabaya.

    DR Congo ni mojawapo ya nchi maskini zaidi duniani, licha ya rasilimali zake nyingi za madini.

    Pia imekumbwa na migogoro ya kivita mara kwa mara.

  7. Mlipuko wa lori la mafuta wauwa zaidi ya watu 40 nchini Liberia

    xx

    Chanzo cha picha, LIBERIA NATIONAL RED CROSS SOCIETY/FACEBOOK

    Zaidi ya watu 40 wamefariki dunia baada ya lori la mafuta kuanguka na kulipuka katikati mwa Liberia, afisa mkuu wa matibabu nchini humo Francis Kateh amesema.

    Lori hilo lilianguka kando ya barabara katika mji wa Totota, kilomita 130 kutoka mji mkuu, Monrovia

    Liliwaka moto mara baada ya watu kukimbilia eneo hilo kuchukua mafuta kutoka mafuta, walioshuhudia walisema.

    Mwanamke mjamzito alikuwa miongoni mwa waliofariki, na baadhi ya miili ilichomeka hadi ikasalia majivu, Dk Kateh alisema.

    Akizungumza na kituo cha Super Bongese TV alisema watu 83 wamelazwa hospitalini kutokana na majeraha waliyopata katika mkasa huo wa Jumanne.

    Waathiriwa waliokuwa na majeraha mabaya zaidi wamehamishiwa katika hospitali za Monrovia kwa matibabu, Dkt Kateh aliongeza.

  8. Mzozo wa Sudan: Mkutano wa ana kwa ana kati ya majenerali wanaozozana waahirishwa Djibouti

    xx

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mazungumzo ya ana kwa ana kati ya viongozi wa makundi yanayopigana nchini Sudan yanayotarajiwa kufanyika siku ya Alhamisi katika taifa dogo la Afrika Mashariki la Djibouti yameahirishwa hadi mwezi ujao kutokana na "sababu za kiufundi."

    Tarehe sahihi ya mazungumzo bado haijabainishwa, mamlaka nchini Djibouti imesema.

    Huu ungekuwa mkutano wa kwanza kati ya wapinzani Jenerali Abdel Fattah al Burhan wa Jeshi la Sudan (SAF) na Jenerali Mohamed Hamadan Dagalo, mkuu wa kundi la wanamgambo la Rapid Support Forces (RSF) tangu mapigano yalipozuka mwezi Aprili.

    Maelfu ya watu wameuawa tangu wakati huo na zaidi ya watu milioni saba wamefukuzwa makwao katika kile ambacho Umoja wa Mataifa ulikiita "mgogoro mbaya zaidi duniani wa kuhama makazi."

    Wakati huo huo mapigano yaliendelea kuripotiwa katika mji mkuu Khartoum.

    Katika hali nadra tangu kuanza kwa mzozo huo,

    Jenerali Dagalo amesafiri hadi Uganda na kukutana na kiongozi wa nchi hiyo Rais Yoweri Musevinina baadaye kuelekea mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa ambako alikaribishwa na naibu waziri mkuu.

    Maelezo zaidi:

  9. Vita vya Israel na Gaza: Waziri wa Israel aonya Hezbollah kuhusu mashambulizi mpakani

    Benny Gantz, kiongozi wa upinzani, alikubali kuingia katika serikali ya dharura na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu baada ya mashambulizi ya Oktoba 7.

    Chanzo cha picha, Reuters

    Jeshi la Israel litachukua hatua ya kuiondoa Hezbollah kwenye mpaka na Lebanon iwapo mashambulizi yake yataendelea, waziri wa Israel ameonya.

    Benny Gantz alisema IDF itaingilia kati ikiwa ulimwengu na serikali ya Lebanon haitawazuia wanamgambo kufyatua risasi kaskazini mwa Israel.

    Wakati wa suluhu la kidiplomasia ulikuwa ukiisha, aliongeza.

    Majibizano makali ya risasi yamekuwa yakiongezeka tangu Hamas iliposhambulia Israel tarehe 7 Oktoba.

    Hali hii imesababisha wasiwasi kwamba mzozo wa Gaza unaweza kuwa mpana katika eneo lote.

    "Hali kwenye mpaka wa kaskazini wa Israel inadai mabadiliko," Bw Gantz aliuambia mkutano wa waandishi wa habari Jumatano usiku.

    Amesema kama dunia na serikali ya Lebanon haitachukua hatua ili kuzuia kufyatuliwa risasi kwa wakazi wa kaskazini mwa Israel, na kuwaweka mbali na mpaka Hezbollah, IDF itafanya hivyo."

    Bw Gantz, mwanasiasa wa upinzani na kiongozi wa zamani wa jeshi la Israel, alijiunga na baraza la mawaziri la vita la Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kama waziri asiye na wizara maalum kufuatia mashambulizi ya Hamas.

  10. Waziri wa Zambia ajiuzulu kwa madai ya kuonekana kwenye video akipokea fedha

    Stanley Kakubo

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Zambia Stanley Kakubo amejiuzulu baada ya kudaiwa kunaswa kwenye video akipokea rundo la fedha kutoka kwa mfanyabiashara wa China.

    Hakukana kuwa alikuwa kwenye video. Badala yake, Bw.Kakubo alisema anakabiliwa na "madai mabaya kuhusu shughuli za kibiashara" na amejiuzulu ili serikali "isikengeushwe" na utata huo.

    Video hiyo inawaonesha wanaume wawili wakiwa wameketi kando ya meza wakihesabu pesa zilizopangwa vizuri, dola za Marekani na kwacha ya Zambia.

    Nyuso zao hazionekani, lakini ilisababisha tetesi kwenye mitandao ya kijamii kwamba watu hao walikuwa Bw Kakubo na mfanyabiashara wa China.

    Baadhi ya watu walihoji kwa nini uhamishaji fedha kwa njia ya benki haujafanywa na ikiwa ushuru ulikuwa umelipwa kufuatia muamala huo.

    Picha ambazo hazijathibitishwa za noti zilizosainiwa kwa mkono pia zilijitokeza kwenye mitandao ya kijamii.

    Mmoja alisema kuwa dola 100,000 "zimebadilishwa" kati ya Mzambia na kampuni ya uchimbaji madini ya China. Mwingine, wa tarehe 8 Julai 2022, alitaja jumla ya $200,000.

    Katika barua yake ya kujiuzulu, Bw Kakubo hakupinga uhalisi wa video hiyo au maelezo yaliyoandikwa kwa mkono, badala yake, alisema alikuwa mwathirika wa "madai ovu juu ya shughuli za kibiashara kati ya biashara yangu ya binafsi ya familia na mshirika wetu wa kibiashara ambaye bado tuna uhusiano mzuri naye".

    Alisema amejiuzulu uwaziri ili kuhakikisha kuwa serikali "haibabaishwi" na juhudi zake za kuboresha maisha ya Wazambia, lakini atabaki kuwa mbunge.

    "Kwa wakati ufaao, tutatoa muktadha sahihi unaozunguka matukio ya hivi karibuni," tovuti ya habari ya Lusaka Times ilimnukuu Bw Kakubo akisema. Bw Hichilema alikubali kujiuzulu kwake, akisema anatambua "kazi na uongozi wa Bw Kakubo unaotukuka".

    Hii ni mara ya pili kwa Bw.Kakubo kujipata katikati ya mabishano.

    Mwaka jana, alishtakiwa kwa kupokea rushwa baada ya kuonekana akitoka katika ofisi ya kampuni ya saruji inayomilikiwa na Wachina.

    Alikanusha kufanya makosa yoyote, huku rais akimtetea akisema amepokea kalenda na shajara.

    Kampuni za China ni wawekezaji wakubwa nchini Zambia. Ubalozi wa China ulisema mwaka 2022 kuwa zaidi ya biashara 600 za China zimewekeza zaidi ya $3bn nchini Zambia.

    Bw Kakubo ndiye waziri wa kwanza kulazimishwa kujiuzulu tangu Rais Hakainde Hichilema aingie madarakani Agosti 2021. Bw Hichilema aliahidi kupambana na ufisadi, lakini upinzani unamshutumu kwa kuwalenga isivyo haki wanachama wake, jambo ambalo anakanusha.

  11. Antony Blinken awaongoza maafisa Mexico kujadili wimbi la wahamiaji

    Rais Lopez Obrador na Antony Blinken walikutana Mexico kushughulikia ongezeko la uhamiaji.

    Chanzo cha picha, EPA

    Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amefanya mazungumzo na Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador, huku mzozo unaoongezeka wa wahamiaji ukisababisha ghasia kwenye mpaka wao wa pamoja.

    Mkutano huo wa ngazi ya juu ulikuja huku shinikizo likiongezeka kwa Ikulu ya White House kukomesha wimbi la wahamiaji nchini Marekani.

    Maafisa wa Marekani walisema wiki iliyopita kuwa hadi watu 10,000 walikuwa wakivuka mpaka wa kusini kila siku.

    Bw Lopez Obrador yuko tayari kuwawekea kikomo watu wanaovuka Mexico kuelekea Marekani. Lakini, akizungumza kabla ya mkutano huo wa kilele katika mji mkuu wa nchi yake, Mexico City, alitoa wito kwa juhudi zaidi kushughulikia sababu za msingi za uhamiaji na kuonya kwamba inaweza kuwa suala muhimu katika uchaguzi wa 2024 wa Marekani.

    Rais wa zamani Donald Trump amechukua msimamo mkali kwenye mpaka na inaripotiwa kuwa ataanzisha msako mkali dhidi ya wahamiaji wasio na vibali ikiwa atarejeshwa ofisini mwaka ujao.

    "Lazima tuchukue tahadhari, kwa sababu wanakampeni hutumia suala hili kama kilio," Bw Lopez Obrador aliwaambia wanahabari. "Ni ufanisi zaidi na utu zaidi kuwekeza katika maendeleo ya watu na ndivyo tumekuwa tukipendekeza."

  12. Mshambuliaji akiri kuua mwanaume mmoja na mtoto wake kabla ya kufanya shambulizi chuoni

    Kozak ambaye pia alimuua baba yake, alifanya idadi ya waathiriwa kufikia 17

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mshambuliaji aliyewaua watu 14 katika chuo kikuu huko Prague alikiri mauaji ya awali mara mbili katika barua yake kabla ya kifo chake, polisi wa Czech wamesema.

    Barua iliyopatikana katika nyumba ya David Kozak ilikuwa ya kukiri kwamba alimpiga risasi mwanaume na mtoto wake wa kike katika msitu karibu na jiji mnamo 15 Desemba, siku sita kabla ya shambulio la Chuo Kikuu cha Charles.

    Polisi walisema amekuwa kwenye orodha ya washukiwa 4,000 wa mauaji.

    Kozak ambaye pia alimuua baba yake, alifanya idadi ya waathiriwa kufikia 17.

    Shambulizi katika chuo kikuu tarehe 21 Disemba ni shambulio baya zaidi katika historia ya Czech.

    Kozak, mwenye umri wa miaka 24 mwanafunzi wa shahada ya uzamili katika chuo kikuu hicho, alijiua baada ya kuzingirwa na polisi waliokuwa wamejihami.

  13. Vita vya Ukraine: Marekani yatoa msaada wa mwisho wa kijeshi kwa Kyiv

    Mwanajeshi wa Ukraine

    Chanzo cha picha, Reuters

    Ikulu ya White House imeidhinisha awamu nyingine ya msaada wa kijeshi wa Marekani kwa Ukraine wenye thamani ya takribani $250m (£195m).

    Msaada wa hivi punde zaidi ni pamoja na ulinzi wa anga, mizinga na risasi za silaha ndogo ndogo, na silaha za kukinga vifaru, maafisa wa Marekani wanasema.

    Lakini inaashiria ufadhili wa mwisho unaopatikana bila idhini mpya kutoka kwa Congress, ambapo mazungumzo yamekwama.

    Ukraine imeonya kwamba juhudi za vita na fedha zake za umma ziko hatarini ikiwa msaada zaidi wa Magharibi hautapatikana.

    Ingawa juhudi za vita vya Ukraine zina uungwaji mkono mkubwa katika Bunge la Marekani, makubaliano kuhusu silaha zaidi yamesitishwa na Warepublican ambao wanasisitiza kuwa hatua kali zaidi za usalama kwenye mpaka wa Marekani na Mexico lazima ziwe sehemu ya mpango wowote wa msaada wa kijeshi.

    Hatua ya matumizi ya dharura ambayo ingetoa $50bn kwa Ukraine na $14bn kwa Israeli ilishindwa katika Seneti mapema mwezi huu, na kila mwanachama wa Republican akipiga kura dhidi yake, pamoja na Bernie Sanders, mtu huru ambaye kwa kawaida hupiga kura na Democrats lakini ameelezea wasiwasi wake kuhusu. Vita vya Israeli dhidi ya Hamas.

    Ziara iliyofuata ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ilishindwa kuwashawishi wabunge.

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken alisema katika taarifa yake akitangaza mpango huo wa msaada kwamba "ni muhimu kwamba Bunge la Congress lichukue hatua haraka iwezekanavyo, ili kuendeleza maslahi yetu ya usalama wa taifa kwa kuisaidia Ukraine kujilinda na kulinda mustakabali wake".

    "Msaada wetu umekuwa muhimu katika kusaidia washirika wetu wa Ukraine wanapolinda nchi yao na uhuru wao dhidi ya uvamizi wa Urusi," aliongeza.

    Mapema mwezi huu msaada wa Euro bilioni 50 kwa Ukraine ulizuiwa na Hungary.

    Ukraine inakabiliwa na nakisi ya bajeti ya $43bn na maafisa wanasema wanaweza kuchelewesha mishahara na pensheni kwa wafanyakazi wa serikali ikiwa msaada zaidi kutoka kwa Magharibi hautakuja hivi karibuni.

  14. Habari za asubuhi, karibu katika taarifa zetu za moja kwa moja