Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Pambano la Kwanza la ngumi baada ya miaka 60 Visiwani Zanzibar
Mamia ya mashabiki wa masumbwi visiwani Zanzibar walijitokeza usiku wa kuamkia leo kushuhudia pambano la kwanza la masumbwi baada ya marufuku ya mchezo huo kudumu kwa takriban miongo sita.
Marufuku ya masumbwi iliyotolewa 1964 kutokona na sababu za kitamaduni.
Hata hivyo marufuku hiyo iliondolewa Septemba mwaka jana na serikali ya sasa chini ya Rais wa nane wa Zanzibar, Dkt Hussein Ali Mwinyi.
Mwandishi wa BBC, Alfred Lasteck alihudhuria pambano hilo visiwani Zanzibar na kutuandalia taarifa ifuatayo.