Video inaonyesha wakati ndege ya kivita ya Urusi ilipogonga ndege ya Marekani isiyo na rubani kwenye Bahari Nyeusi
Jeshi la Marekani limetoa picha za ndege ya Urusi ikiangusha moja ya ndege zake zisizo na rubani kwenye Bahari Nyeusi.
Marekani ilisema uharibifu wa ndege hiyo kubwa isiyo na rubani ulimaanisha kuwa ilipaswa kushushwa ndani ya maji karibu na Ukraine siku ya Jumanne.
Urusi ilikanusha kuwa ndege yake ya kivita aina ya Su-27 ilinasa propela ya ndege hiyo isiyo na rubani, lakini video hiyo inaonekana kuunga mkono toleo la Marekani la matukio.
Ilikuwa ni kwa nia ya Pentagon kuachilia video hii - si haba kuthibitisha toleo lake la matukio.
BBC haijaona matukio kabla au baada ya mgongano huo. Hapo awali Marekani ilisema makabiliano hayo yalidumu kwa takriban dakika 30-40.









