‘Wenye ulemavu wa kusikia pia tunaweza kuwa warembo na watanashati'

Mr. & Miss Deaf International ni mashindano ya warembo na watanashati toka pande zote za dunia yanayotarajia kufanyika mwishoni mwa wiki hii nchini Tanzania.

Mwandishi wa BBC @frankmavura ametembelea kambi ambayo walimbwende kutoka Tanzania wamepiga kambi ili kutaka kufahamu machache juu ya ushiriki wao na namna ambavyo mashindano haya yatafanyika.

Je umeshawahi kujiuliza warembo na watanashati hao wanaweza kufuatisha midundo ya sauti? Tazama