Efuoma Amos: 'Kila nikimwangalia mke wangu nabubujikwa na machozi'

Efuoma Amos alizua gumzo mitandaoni baada ya picha zake za kabla ya harusi kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii kutokana na tofauti ya kimo kati yake na mchumba wake.

Mhitimu huyo wa sayansi ya kompyuta alizungumza na BBC Pidgin na kusema haijawahi kupata ugumu wa kuwa kumpata mwanamke yeyote aliyempenda, ''Uwezo wa kuvutia wanawake ni zawadi kutoka kwa Mungu'', alisema.