Freeman Mbowe :Katiba mpya inafaa kuwa kipau mbele kwa Tanzania

Maelezo ya video, Freeman Mbowe :Katiba mpya inafaa kuwa kipau mbele kwa Tanzania

Tanzania itaanza mchakato wa kutunga katiba mpya baada ya uchaguzi mkuu wa 2025.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu inasema katiba mpya itakuwa miongoni mwa masuala mengine ya muda mrefu ambayo yatashughulikiwa wakati huo.

Haya yanajiri baada ya kuachiwa huru kwa kiongozi mkuu wa upinzani nchini humo Freeman Mbowe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Anadai kesi yake mahakamani ilichochewa kisiasa kwa sababu alikuwa ameanzisha vuguvugu la kudai katiba mpya.

Serikali ya Tanzania inakanusha madai hayo na Rais Samia Suluhu katika mahojiano ya awali na BBC alikanusha kuwa kesi hiyo ilichochewa kisiasa na kutaka kuwepo subira ili mahakama kushughulikia kesi hiyo ambapo baadaye mashtaka yote dhidi yake na washtakiwa wenzake yalifutwa .

Katika mahojiano yake ya kwanza na vyombo vya habari, tangu kuachiliwa kwake, Bw Mbowe alizungumza na Salim Kikeke wa BBC

Unaweza poa kusoma/kustazama: