Siku ya wanawake duniani 2022: Wanawake wa Tanzania waliojitosa katika ufundi wa magari

Kutana na Mwasiti Salum na Catherine Kimaro ambao ni wasichana walioamua kujiingiza katika ufundi wa magari wakijikita katika umeme wa magari jijini Dar es Salaam.

Changamoto za maisha na uangaziaji wa fursa za ajira uliwapelekea kutamani kufanya kazi ambayo itawapa pesa ya haraka kujikwamua kiimaisha.

@sittyumeme na @catty_auto_ solution wanapambana na dhana nzima ya ufundi wa magari ni kazi za wanaume peke yao kwa kuuonesha kuwa mwanamke akiamua anaweza.

Video:Frank Mavura