Mzozo wa Ukraine: Wanajeshi wa Ukraine waliofunga ndoa vitani

Huku kukiwa na hofu kubwa ya vita, wapenzi kutoka vikosi vya ulinzi vya eneo la Ukraine wamefunga ndoa, karibu na kituo cha ukaguzi nje kidogo ya mji wa Kyiv.

Katika mazingira hayo yasio ya kawaida , Valery na Lesya, wote wakiwa wamevalia mavazi ya kijeshi walifanya sherehe ndogo wakiwa wamezungukwa na wanajeshi wengine wa Ukraine - na meya wa Kyiv.