Watanzania wanaoishi Ukraine wazungumza kuhusu hali ya hofu iliopo

Mtanzania aliyeopo Ukraine aeleza jinsi hali ilivyo katika mji wa Kharkiv ambapo anasoma masomo yake ya udaktari bingwa. Akizungumza na mwandishi wa BBC Martha Saranga, Dkt. Evans Liseki. Amesema milipuko kadhaa imesikika na. wameamriwa kukaa ndani na mamlaka hivyo ameshindwa kuhudhuria masomo.

Vladimir Putin alitangaza oparesheni ya kijeshi nchini Ukraine saa 5.55 asubuhi majira ya Moscow - na dakikaka chache baadaye makombora ya kwanza yalirushwa Ukraine, kulingana na ripoti.

Katika mji mkuu wa Kyiv, king'ora cha dharura kililia, na picha zinaonyesha msururu wa magari yakifunga barabara ya mwendokasi huku watu wakiukimbia mji huo.