Mambo yanayoendelea katika hifadhi ya wanyamapori ya Ngorongoro yanaibua maswali, mtafiti

Kufuatia hatua ya serikali ya mkoa wa Arusha kupitia mkuu wa mkoa John Mongela hivi Karibuni kutoa maelekezo yanayowaandaa jamii ya wafugaji wa Wamaasai kutakiwa kuondoka katika hifadhi ya Ngorongoro, maoni mseto yameendelea kutolewa kuhusu hatua hiyo.

Jamii ya kimasai inadai kwamba imekuwepo ndani ya hifadhi hiyo kwa miaka mingi bila kuwa na madhara kwa wanyama waliomo humo…wakati ambapo wataalamu wa ikolojia wakitoa sababu za kitaalamu. Mtaalamu wa Ikolojia aliyeko Karatu Tanzania Dr Henry Kenneth Njovu amemuelezea mwandishi wa BBC Martha Saranga ni kwanini mgogoro huo unatokea sasa.