Uchaguzi wa Kenya 2022: Rais Kenyatta na naibu wake Ruto warushiana cheche hadharani

Siku moja tu baada ya Rais Kenyatta kuonekana kumkosoa Bwana Ruto kwa kile anachodai ni kupoteza muda mwingi kwenye mikutano ya kisiasa akifanya kampeni za urais badala ya kuwahudumia wananchi ,leo naibu rais akiwa katika mkutano mwengine wa kisiasa amemjibu bosi wake.

Na wakati huo huo wafuasi wa naibu rais pamoja na Wakenya mbali mbali wakiwemo madaktari na wauguzi wamemkemea katibu mkuu wa chama cha wafanya kazi nchini Kenya Francis Atwoli kwa kudai kuwa Ruto huenda atajinyonga baada ya kushindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.

Odhiambo Joseph na mengi zaidi