Tabu Mtingita: Mwanangu husema mama mi naona aibu unavyochekesha

Katika umri wa miaka 41, Nyota ya @tabumtingita kutoka Tanzania inaonesha nuru katika Sanaa ya uchekeshaji, Licha ya kukabiliana na maoni ya manyanyaso na matusi katika mitandao ya kijamii Tabu hajakata tamaa kuendelea na talanta yake ya uchekeshaji.

Mwandishi wa BBC veronica Mapunda amezungumza na Bi Tabu kujua namna anavyokabiliana na changamoto hizi na jinsi anavyomudu majukumu ya kuwa mama wa mtoto ambaye hafurahii kazi afanyayo mama yake?