Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Binti: Je, filamu ya kwanza ya Kitanzania inayooneshwa Netflix inahusu nini?
Filamu ya BINTI @bintimovie ni filamu ya kwanza ya Kitanzania kuoneshwa katika mtandao wa filamu mitandaoni kwa jina la NETFLIX.
Filamu hiyo inaelimisha mabinti kutotamani maisha ya wenzao ikiwa hawajui wanapitia nini.
Imeandikwa na mtunzi Angela Luhinda pamoja na @sekoshamte na tayari imejinyakulia tuzo katika Zanzibar International Film Festival 2021 .
Ni filamu inayohusu Maisha ya Binti Wa Kiafrika, Kitanzania ikiwa na ujumbe wa kuelimisha mabinti kutotamani maisha ya wenzao ikiwa hawajui ni nini wanapitia.
Imeoneshwa katika majukwaa makubwa ya filamu Kenya, Marekani, Ujerumani miongoni mwa nchi zingine.
Video na @frankmavura