Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya corona: Wanandoa wa Uholanzi waliotoroka karantini wakamtwa
Polisi wa mpakani nchini Uholanzi wanasema wamewakamata wanandoa ambao walikuwa wametoroka hoteli ya karantini karibu na uwanja wa ndege wa Schipol huko Amsterdam.
Maafisa walisema mmoja wao amekuwa akijitenga baada ya kukutwa na virusi vya corona baada ya kusafiri kutoka kutoka Afrika Kusini.
Wenzi hao walifanikiwa kupanda ndege kuelekea Uhispania lakini walikamatwa kabla tu ya kupaa.