Joseph Kabila na kupotea kwa mamilioni ya DR Congo

Ufichuzi wa siri kutoka kwa uvujaji mkubwa wa data za benki, Africa Eye unafichua jinsi mamilioni ya dola za fedha za umma zilivyoishia kwenye akaunti za benki za biashara za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na zinazomilikiwa na familia na washirika wa Rais wa zamani Joseph Kabila.

Uchunguzi huo pia unazua maswali mazito kuhusu miamala ambayo haijaelezewa kupitia akaunti rasmi ya ofisi ya rais wakati Bw Kabila alipokuwa mamlakani.

Uchunguzi huo ni sehemu ya Congo Hold-up, ushirikiano wa kimataifa na upatikanaji wa ushahidi kutoka kwa Benki ya BGFI.