Hekalu la Kotamayasamma : Kwanini pombe na nyama vinatolewa kama sadaka katika baadhi ya madhabahu ya Wahindu?.

Chanzo cha picha, Getty Images
Afisa wa ngazi ya juu nchini India Ram Gopal Varma, aliibua utata baada ya taarifa yake yenye utata kugonga vichwa vya habari hivi karibuni na picha yake kusambazwa kwenye mitandao ya habari ya kijamii. Alikwenda katika eneo la Warangal kwa ajili ya kuchukua picha za filamu pamoja na pombe zilizotolewa kama sadaka hekaluni kwa ajili ya kumpelekea mama yake katika hekalu la Wahindu la Kotamayasamma nchini humo.
Hii iliibua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii pamoja na utoaji wa pombe aina ya whiskey kwa wauzaji hekaluni.
Lakini je vilevi vinauzwa katika madhabahu? Na Je ibada hii hufanyika hekaluni pekee? Utamaduni huu ulianza vipi India?

Chanzo cha picha, TWITTER / RAMGOPALVARMA
Upako wa pombe ...
Utamaduni wa kutoa sadaka ya pombe na vilevi vingi ne katika hekalu haufanyiki kwa hekalu la Kotamayasamma pekee.
'' Pombe kali zinazofahamika kama Liquor hutolewa katika madhabahu mengi ya hekalu nchini India. Kwa mfano katika hekalu la Abbanagunta Mysamma , kuna pombe ambayo humwagwa kwenye mfereji karibu na miguu ya mnunuzi. Lakini tunafanyiwa upako kwa wa pombe, "anasema Kotagandi Ayyappa, kasisi mkuu wa hekalu la Kotamayasamma.
Ayyappa anaeleza kwamba utamaduni huu umekuwa ukiendelea kwa miaka mingi. '' Utamaduni huu umekuwepo tangu nyakati za wafalme. Mwanzoni, hususan mawe yaliyotengenezwa yalikuwa yakitolewa kama sadaka kwenye hekalu .
''Pombe inapaswa kutumiwa wakati mawe hayapo. Kwahiyo utamaduni umeendelea'' , alifafanua.
" Vilevi hutolewa katika hekalu tu lakini pia katika masuala ya vijijini yanayowahusu akina mama na mabinamu ," alisema.
Kwa upande mwingine, Mjumbe wa zamani wa baraza la congress la eneo la MLA Konda Surekha, ambaye hutembelea hekalu kila wiki , "Waumini hutoa sadaka ya mimea pamoja na pombe kali .
Baadhi ya raia wa kigeni pia huleta hekaluni pombe kutoka ng'ambo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Vilevi kwa miungu
Katika maene mengi yan chi ya India, ikiwa ni pamoja nae neo la Telangana, kuna utamaduni wa kutoa vilevi kwa miungu.
Pombe zenye viwango vya juu vya vilevi hutolewa katika Hekalu la Kalabhairav katika Vishweshwara Ganj, mwendo wa dakika kumi kwa miguu kutoka katika hekalu kuu la Vishwanath lililopo Kashi.
Waziri mkuu wa India Narendra Modi alitembelea hekalu hilo kabla ya uteuzi wake katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2019.
Maeneo mengine, zinapotolewa sadaka za vilevi vikali ni katika hekalu za Kalbhairav mjini Delhi, Ahmedabad na Ujjain.
Katika baadhi ya hekalu, tumbaku pia hutumiwa kama sadaka pamoja na vilevi.
Hekalu la Muniyappan ni hekalu la kwanza kwa kutoa muongozo huu ambapo sadaka hizi hutolewa kwa muungu wa kike anayefahamika kama Bhadrakali.
Pombe pamoja na samaki hutolewa pia katika Hekalu la Parassinikadavu Muthappan lililopo eneo la Kerala.
Utamaduni huu ulianza vipi?
Mwanahistoria Dwijendra Narayan Jha anasema utamaduni wa kutoa sadaka na matambiko ya pombe katika hekalu za dhehebu la Hindu ulianza zama za Vedic ( c. 1500 - c. 500 BCE)
Katika kipindi cha Vedic , aliandika kitabu kuhsuu utamaduni huu "Drinks of Immortality (ua Vinywaji vya kutokufa), Makala iliyoelezea kuhusu matumizi ya vilevi katika India ya kale ".
'' Soma pia alikuwa ni mmoja wa miungu walioabudiwa katika kipindi Vedic . Soma ipia ni jina la pombe iliyotengenezwa kutokana na mti uliopewa jina lake.
Inasemekana pombe hiyo ilikuwa ikitplewa kama sadaka kwa .
Sura pia ni kilevi
"Ulevi wa miungu…mara kwa mara hutajwa katika historia kuhusu miungu wa kale nchini India ."

Chanzo cha picha, DRINK OF IMMORTALITY
Vilevi pia ni sadaka mojawapo inayopendwa sana na miungu wanaoabudiwa na Wahindu. Sadaka haitimii bila pombe unapowaabudu na kutoa sadaka au matoleo kwenye madhabahu'' anasema msomi wa dini ya Hindu.
Mwandishi wa habari mstaafu Clock Dhruvakumar Maitreya pia anakubaliana na kauli za Mwanahistoria Dwijendra Narayan Jha. '' Ibada hii ya kutoa sadaka ya vilevi imekuwepo India tangu nyakati za Vedic. Kila mara tunasikia kuhusu sadaka ya vilevi.
Wakati mwingine, mawe ya aina sita, mimea kama vile mti wa mtende vinatolewa kwenye hekalu pamoja na maua, "alielezea Dhruvakumar.

Chanzo cha picha, Getty Images
Hata nyama hutolewa hekaluni…
Katika baadhi ya hekalu, Wanyama hutolewa kama matambiko na na nyama hutgawiwa kama sadaka . Dhruvakumar alisema kuwa utamaduni huu pia ulianza yakati za kale za Vedic.
"Wanyama walikuwa wanatolewa kafala katika ibada za kale. Nyama zilikuwa zinatolewa kwa kila mtu. Utamaduni huu unaendelea.
Utamaduni huu bado upo katika hekalu nyingi za vijijini nchini India. Wakati wa matamasha, wanyaa wanatolewa kafala kwa miungu na nyama hutolewa kama sadaka, " alielezea

Chanzo cha picha, Getty Images
Kitu kingine…kwamfano, nilipohamia katika nyumba mpya, kila mtu alikuwa anaabudu miungu kama vile Ellamma, Paddamma na Mysamma. Lakini ukihamia katika nyumba mpya leo inamaanisha kwamba utoaji wa kafala kwa mungu Satyanarayana vratham ni jambo la lazima. Hivi ndivyo watu wengi wanavyoitazama miungu. Tamaduni kuhusu miungu hii imebadilika kadri miaka inavyokwenda , "alieleza.









