Wanawake wa Malawi wanaobadilisha uchafu kuwa fedha

Mji mkuu wa Malawi Lilongwe lenye maenedeleo chungu nzima yanayochipuka na mitaa yenye shughuli nyingi.

Lakini mbali na hilo ni mji wenye na tatizo kubwa la usimamizi wa taka.

Hivyobasi kikundi kimoja cha wanawake katika eneo lenye wakazi wengi la Kawale kinafanya kazi ya kubadilisha hali ya usafi katika jiji hilo.

Wao hukusanya taka ambazo hubadilishwa na kuwa rasilimali inayotumika.