Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Hushppupi: Fahamu alivyotajirika na kuwa milionea na baadaye kukamatwa
Ramon Abbas – maarufu Hushpuppi kama anavyofahamika na mamilioni ya msahabiki wake mtandaoni- amekiri kosa la utakatishaji fedha katika mahakama ya Marekani.
Mshawishi huyo wa mitandao ya kijamii na raia wa Nigeria alipata umaarufu kutokana na mtindo wake wa maisha, kwa kuvalia nguo za bei ghali na kujionesha anavyojivinjari katika sehemu za kifahari na magari ya bei ghali kwa wafuatiliaji wake milioni 1.3 kwenye Snapchat.
Lakini mashabiki wake hawakujua mtindo huo wa maisha ulifadhiliwa kupitia uhalifu wa mtandaoni.