Rais Kenyatta atetea ajenda yake ya kuleta umoja nchini Kenya
Uhuru aliongeza kuwa alishangaa kwanini naibu wake alikuwa akipinga mchakato wa BBI akisema "maswala yaliyopelekea kuundwa kwa BBI ndio yaleyale yaliyowaleta pamoja".
"Ikiwa ninataka sasa kupanua hilo, kuna shida? Tukirudi nyuma hadi mwaka wa 2013 imekuwa ajenda yangu ya kuleta watu pamoja," Uhuru alisema. "Ikiwa mgawanyiko wa 2007 ulituleta pamoja, kuna shida tukiwaleta watu wengine ndani?" alihoji
Rais alihimiza utulivu akisema hatua yake ya kuiunganisha nchi haimaanishi kupunguza nafasi za mtu yeyote kumrithi.
"Haikunyimii nafasi zako Sio Uhuru anayechagua, ni Wakenya."
Alijutia pia kwamba maswala kadhaa yaliyosababisha mgawanyiko ambao umetikisa utawala wake yanatokana na ari yake ya kuleta umoja .
"Kuna shida gani ikiwa tuna hali ya kila mtu kujumuishwa ...ambayo haijalishi ni nani atashinda, hakuna Mkenya aliyepoteza?" Aliuliza.
Alikuwa akizungumza katika mahojiano na runinga ya Citizen wakati wa mkutano na wahariri nchini humo