Wagner:Jeshi la mamluki linalodaiwa kufadhiliwa na Urusi

Maelezo ya video, Mamluki nchini Libya: 'Huu ni ufalme wa mlengaji shabaha wa Urursi'

Libya imekumbwa na mzozo tangu mwaka 2011, wakati Kanali Muammar Gaddafi aling’olewa madarakani.

Tangu wakati huo, serikali mbili ambazo zimekuwa zikihasimiana zimegawanya nchi hiyo kuwa magharibi na mashariki.

Muingilio wa nchi za kigeni umekuwa na athari kubwa katika vita hivyo, kwani pande zote mbili zinaungwa mkono ma mataifa ya kigeni, ikiwa ni pamoja na Urusi na Uturuki.

BBC Idhaa za Kiararu na Kirusu zimechunguza kwa miezi kadha jukumu la mamluki wa Urusi wa Kundi la Wagner, na zimefanikiwa kuwatambua wawapiganaji wa Urusi ambao wamekuwa wakifanya kazi upande mmoja wa vita. Uchunguzi pia umefichua ushahidi wa uhalifu wa kivita ambao unashukiwa kutekelezwa na kundi hilo nchini Libya