Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Naibu wa rais wa Kenya apasua mbarika baada ya kuzuiliwa kwenda Uganda
Naibu wa Rais wa Kenya Wiliam Ruto hatimaye amezungumzia kisa cha Jumatatu ambapo alizuiliwa kusafiri nchi jirani ya Uganda kwa ziara ya kibinafsi .
Katika mahojiano na kituo cha Radio cha Inooro kinachomilikiwa na Kampuni ya Royal Media, Bwana Ruto alisema kufutwa kwa safari yake ni hatua ya kumdunisha akisimulia changamoto alizopitia yeye na washirika wake.
''Tuna shida. Wabunge wengi wamefukuzwa katika kamati za bunge. Nimewekwa pembeni. Kwa hivyo, kile kilichofanyika (katika Uwanja wa Ndege wa Wilson) ilikuwa hatua ya kunidhalilisha na kunifanya nionekane sina maana'', alisema.
Licha ya kuvunjika kwa safari yake anasema mkutano uliokuwa ahudhurie uliendelea.