Watanzania wana maoni yapi kuhusu kupokea chanjo ya Corona?

Tanzania imepokea dozi yake ya kwanza ya chanjo ya Corona mwishoni mwa juma wakati huu muongozo mpya wa kukabiliana na Corona ukitangazwa na wizara ya afya nchini humo.

Utekelezaji wake unabaki kuwa kitendawili huku hatua gani haswa zitakazochukuliwa dhidi ya watakaokiuka utaratibu wa kupambana na Covid19 zikisalia kuwa swali la msingi.

Lakini Watanzania wana maoni gani juu ya kupokea kwa chanjo hii?