Mbona maelfu ya wahamiaji wa Ethiopia hufanya safari hatari na ndefu kwenda Saudi Arabia?

Kila mwaka makumi ya maelfu ya Waethiopia huanza safari hatari ya kilomita 2000 kutoka nchi yao kwenda Saudi Arabia, wakijaribu kuvuka milima, jangwa, Bahari ya Shamu na hata eneo linalokumbwa na vita .

Baadhi ya wahamiaji hawa wanaelezea jinsi wanavyokabiliwa na wizi, utapeli na njaa katika joto la zaidi ya nyuzi joto 50.

Haishangazi wengi hufa njiani, wakati wengine wanazidiwa na kushindwa kumaliza safari wakibakia kuomba mitaani

BBC Africa Eye inakuletea simulizi ya baadhi ambao huhatarisha maisha yao kufanya ziara hiyo kwa matumaini ya kupata maisha mazuri.