World Albinism Day: Baba yangu alisema hawezi kumlea mtoto ‘anayefanana na nguruwe’
Isaac Mwaura ndiye mtu wa kwanza Kenya mwenye ulemavu wa ngozi kuwahi kuwa mbunge na seneta . Licha ya kuachwa na babake akiwa na umri wa miaka minne kwasababu ya kuzaliwa akiwa Albino ,Mwaura hajafa moyo na amekuwa mstari wa mbele kuyatetea maslai ya wau wenye ulemavu wa ngozi .
Anasema babake alikataa kuendelea kumpa malezi akidai kwamba ‘hakutaka kumlea mtoto aliyefanana na nguruwe’. Mwaura anasema huo ndio uliokuwa mwanzo wa kasumba ya kuonekana tofauti au kudhalilishwa na kwa namna fulani ni jambo ambalo limempa msukumo wa kutaka kuwasaidia watu wengine waliozaliwa na ualbino .
‘Sijawahi kukutana na babangu.. nimejaribu kumsamehe babangu ,kuna pengo ambalo ziwezi kuliziba .Kila mtoto anafaa kulelewa na wazazi wake wote na watoto wengi wenye ulemavu wa ngozi wamelelewa na mama zao pekee’ anasema Mwaura .
Mwaura anaishauri jamii kubadiisha dhana kwamba wtau wenye ulamavu wa ngozi wana udhaifu fulani wa kutoweza kuafikia ama kutekeleza majukumu kama watu wengine .Anasema kando na sababu ambazo ni za wazi ,watu wenye hali hiyo wana uwezo wa kunawiri katika majukumu mbali mbali na hata kazi ambazo watu wa kawaida wanazifanya .
‘ Watu wanafikiri kwamba watu wenye hali hii hawajiwezi kwasababu ya hilo na ukijitokeza kwa ukakamavu kufanya jambo wanasema basi ….wewe nsi mlemavu’
‘ Iwapo utazaa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi basi hakikisha kwamba unahusika na maisha yake na usimuache .

