Joanné Dion: Watu weusi wanafikiri ninapendelewa kama Wazungu
Mwanamitindo mwenye ualbino Joanné Dion amepigania kufanana na jamii inayomzunguka ambapo mara nyingi amekuwa na changamoto ya kutokubalika na jamii ya watu weusi na weupe.
Alizaliwa akiwa albino, alipokuwa akikua amekuwa akizomewa na kuitwa majina kama Casper yule Mzuka na poda aina ya talcum
Amepigania sana kupata nafasi ya kuwa mwanamitindo na ameiambia BBC : ‘’Siko sawa, na ninaona sawa tu’’