Sheikh Jarrah: Eneo ambako Wayahudi hawataki Wapalestina waishi

Kutishiwa kufurushwa kwa familia kutoka kwenye nyumba zao katika eneo la Sheikh Jarrah ilikuwa mojawapo ya sababu zilizoibua makabiliano ya hivi karibuni kote Israeli na Gaza. Mali zilizopo katika eneo hili zinadaiwa na kundi la walowezi wa Kiyahudi katka mahakama za Israeli. Mahakama ya juu zaidi ya Israeli iliahirisha kusikiliza kesi. Lakini je ni upi hasa msingi wa kisheria wa madai haya?...Yossi Melber kutoka taasisi ya Chatham House ya masomo ya sera anaelezea kwa kina kesi hii