Virusi vya corona: 'Hatuna nafasi ya kuichoma miili', raia wa India waeleza

Idadi ya vifo kutokana na janga la corona imeongezeka kwa kiasi kikubwa nchini India, kukiwa na upungufu wa dawa na oksijeni.

Familia zimekuwa zikisubiri kwa saa nyingi-siku kadhaa- kufanya taratibu zao za mwisho za kuchoma miili ya wapendwa wao kutokana na ukosefu wa nafasi kwa ajili ya shughuli hiyo.

Jumatatu India ilirekodi maambukizi makubwa kwa siku ikiwa ni siku ya tano mfululizo na kufika idadi ya watu 352,991 na imeendelea kushuhudia idadi hiyo ikiongezeka kila siku.