Kwanini Kenya inasisitiza kuhusu uhifadhi wa mazingira ya Kasa wa baharini Malindi?

Ukijulikana kwa umaarufu wake wa michanga myeupe na hoteli za kifahari, mji wa Malindi uliopo katika pwani ya Kenya na kaskazini mwa mji wa kitalii wa Mombasa upo katikati ya juhudi za serikali ya Kenya kuamua kuhusu ujenzi zaidi wa hoteli za kifahari katika kilomita 530 ya pwani yake na kulinda Maisha ya Wanyama wanaoishi baharini.

Hivyobasi tunauliza je! Ni kweli kwamba hakuna kitu muhimu kinachoweka wazi tatizo la ikolojia ya Kenya kuliko ulinzi wa kasa wa baharini? BBC Afrika ilienda Watamu , kaskazini mwa mji wa pwani wa Mombasa kubaini ukweli.