Uchaguzi Uganda 2021:Waangalizi wa Afrika Mashariki wasema uchaguzi ulikuwa wa huru na haki

Maelezo ya video, Waangalizi wa Afrika Mashariki wasema uchaguzi ulikuwa wa huru na haki

Kundi moja la waangalizi wa uchaguzi limesema kuwa uchaguzi mkuu wa Uganda ulikuwa huru na wa haki.

Waangalizi wa Afrika Mashariki, EASF, linasema kwa ujumla uchaguzi uliongozwa kwa njia ya amani, bila purukushani wala ghasia.

Lakini kundi hilo limesema kuzimwa kwa mtandao wa intaneti kuliwanyima raia wa Uganda uhuru wa kujieleza.

Mwanahabari wetu Roncliffe Odit amezungumza na Bi Irene Ogaja wa kundi hilo la waangalizi la EASF.