Xavier Hopkins: Mwendeshaji baiskeli mwenye upofu afadhiliwa kusafiri duniani

Xavier Hopkins anapanga kuwa mwendeshaji baiskeli wa kushuka milima licha ya kwamba uwezo wake wa kuona ni asilimia 10.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 20 kutoa eneo la Reading ana tatizo la macho linayoyafanya kuchezacheza mara kwa mara.

Na baaada ya kushindwa kupata kazi aliamua kuchukulia kazi ya uendeshaji baiskeli na umuhimu mkubwa.

Hivi sasa amefadhiliwa kusafiri barani Ulaya akihudhuria maonesho ya uendeshaji biaskeli baada ya kuchapisha video akiendesha baiskeli mtandaoni.