Uchaguzi Tanzania 2020: Mkurugenzi wa uchaguzi Zanzibar azungumzia madai ya changamoto ya vitambulisho vya mpigakura

Taifa la Tanzania linatazamiwa kufanya uchaguzi wake mkuu wenye kuhusisha madiwani, wabunge na rais ifikapo October 28 Mwaka huu.

Ni uchaguzi wa Tanzania bara na visiwani. Hata hivyo kila mpiga kura atatakiwa kuwa na kitambulisho ili kumuwezesha kushiri haki yake ya kimsingi ya kupiga kura.

Lakini visiwani Zanzibar, suala la vitambulisho vya mpiga kura limekua tata.

Mkurugenzi wa Uchaguzi Zanzibar Thabit Faina Amezungumza na mwandishi wetu Aboubakar Famau, na kwanza amemuuliza kuhusu malalamiko ya baadhi ya wananchi kwamba mpaka sasa hawajapata vitambulisho hivyo.