'Kichwa na viungo vinaniuma sana nyakati za mchana'

Maelezo ya sauti, 'Kichwa na viungo vinaniuma sana'

Mwanahabari wa Kenya Yasin Juma, ameachiliwa huru kutoka gerezani nchini Ethiopia alipokuwa akishikiliwa tangu mwezi Julai mwaka huu.

Mwanahabari huyo amekuwa akizuiliwa na polisi tangu kutokea kwa maandamano ya ghasia Ethiopia kufuatia kuuawa kwa mwana muziki ambaye na mwanaharakati wa jamii ya Oromo Hachalu Hundessa.

Hata hivyo kumekwa na taarifa kwamba mwanahabari huyo wa Kenya ameshindwa kurejea nyumbani kwa madai kwamba ameambukizwa virusi vya corona na kwa sasa karantini.

Mwandishi wa BBC Regina Mziwanda amezungumza na mwanahabari huyo- Yassin Juma.