Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wito wa BBC wa muziki wa kuwasaidia wagonjwa wa kusahau
BBC imezindua mpango wa kusisimua kwa mashabiki wake duniani, na bila shaka wewe pia unaweza kuwa sehemu ya mpango huo. Siku ya kimataifa ya Alzheimer inayoadhimishwa Septemba 21 – Tovuti ya BBC Swahili itakusanya nyimbo bora za mapenzi kutoka kila pembe duniani. Tusaidie kuchagua nyimbo 50 murua za Kiswahili au ya kitamaduni kutoka nchini mwako ili tuandae orodha ya muziki unaomilikiwa na wewe. Tuma chaguo la muziki wako, kutoka nchi gani au umeimbwa kwa lugha gani kwa bbc.swahili.com. Muziku huo utatusaidia kubuni urodha ya muziki maalum kwa wapendwa wako.