Simon Sirro: Tunachunguza bilioni 6 za Tanzania zilizoingia katika akaunti hiyo

Mtandao wa Watetezi wa haki za Binadamu Tanzania, THRDC umeamua kufunga shughuli zake nchini humo baada ya akaunti zake za benki kufungiwa na polisi.

Kutokana na taarifa yao Mratibu wa Mtandao Onesmo Olengerumwa aliitwa kwa mahojiano na polisi kuhusu tuhuma za taasisi kutokuwasilisha mikataba yake ya wafadhili wa taasisi katika Ofisi ya Hazina na Ofisi ya Msajili.

Baadae aliachiwa kwa dhamana ya watumishi wawili wa umma kwa bondi ya shilingi milioni 200 za Kitanzania. Kutaka kufahamu zaidi naungana na Inspekta Jenerali wa Polisi Tanzania Kamanda Simon Sirro.