Waandamanaji Kenya watawanywa kwa mabomu ya kutoa machozi

Wakati nchini Tanzania polisi wakitahadharisha kutofanya maandamano, huko kenya vitoa machozi vimetumika kusambaratisha maandamano ya sabasaba.

Maandamano ya sabasaba yanafanyika Kenya ikiwa ni miaka 30 ya saba saba, siku ambayo kulikuwa na maandamano nchi nzima Kenya mwaka 1990 kudai demokrasia ya vyama vingi kutoka kwa utawala wa Rais Moi.