Virusi vya corona: BBC Africa Eye yabaini jinsi corona inavyoathiri maisha Sierra Leone

Sierra Leone ilikuwa ni moja ya nchi zilizoathiriwa vibaya wakati mlipuko wa ugonjwa wa Ebola ulipoyakumba mataifa ya Magharibi mwa Afrika mwaka 2014.

Sasa inakabiliana na virusi vya corona. Mtu wa kwanza alithibitishwa kupata maambukizi tarehe 31 Machi na tangu wakati huo idadi ya maambukizi imekua ikiongezeka. Tyson Conteh ni mtengenezaji wa filamu katika mji wa Makeni uliopo kaskazini mwa Sierra Leone. Aliangazia mlipuko wa Ebola kwa ajili ya BBC Africa Eye katika Makala iliyoitwa Standing Among The Living na sasa anaandaa msururu wa video kwa ajili ya BBC Africa Eye akionesha ni jinsi gani jiji lake linakabiliana na virusi vya corona.

Katika awamu ya nne, ya video hizi, tunaangalia namna athari za amri ya kutotoka nje nchini humo ilivyoathiri uwezo wa watu kujilisha. Tyson anakutana na kikundi cha wafanyabiashara ya ngono wanaoamini nja inaweza kumuua mtu haraka kuliko virusi vya corona na kwahiyo wanaendelea kufanya kazi.

Waandaaji:

Imeongozwa na Tyson Conteh na Video imechuliwa na Chernor Mustapha Thoronka (Justice), The Future View Media Centre katika Makeni.

Imetengenezwa na kuhaririwa na Jerry Rothwell na Sam Liebmann, Metfilm Production.

Muziki umetolewa na Purple Field Productions PFP.