Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mwanandondi wa kulipwa wa kwanza mwanamke nchini Zimbabwe anayewaasa watu kusamehe
Monalisa Sibanda ni mwanandondi wa kulipwa wa kwanza mwanamke nchini Zimbabwe.
Alijinyakulia taji la mwanandondi wa mwaka 2019 la Shirikisho la kimataifa la Ndondi la Wanawake (WIBA), akiwa ni mwanamke wa kwanza Zimbabwe kupata taji hilo.
Wakati akitaka kulipiza kisasi kutokana na kifo cha mama yake, Monalisa alianza ndondi kujilinda pamoja na wanawake wengine. Kutokana na mafanikio yake katika mchezo ambao kwa kawaida huchezwa zaidi na wanaume, anawashauri wanawake wengine kusamehe na kuendelea na maisha ya kujiendeleza wenyewe.