Wahamiaji haramu watumia muziki kusahau shida zao Italia

Yankuba ni kijana wa Gambia ambaye alitoroka ukandamizaji na kuanza safari ya kutisha baharini na ardhini hadi Ulaya.

Alipofika Napoli , aligundua mazingira magumu ya ubaguzi wa rangi mbali na idara ya uhamiaji isiopendelea wahamiaji.

Alilazimika kutoroka na kujificha katika klabu moja ya burudani katika mji unaoitwa Teranga.

Klabu hiyo inatoa fursa isio ya kawaida kwa wahamiaji kucheza densi na kuimba ili kukabiliana na maumivu ya safari yao ya kuelekea Ulaya mbali na ubaguzi wa rangi wanaokabiliana nao chini Itali.