Virusivya corona: Wafanyabiashara wa Tanzania wailalamikia Zambia

Janga la Corona limeathiri kwa kiasi kikubwa shughuli za kibiashara katika mji wa Tunduma ambao uko kwenye mpaka wa Tanzania na Zambia.Wakazi wa eneo hilo wana hofia huenda hali ikazorota zaidi baada ya Zambia kuufunga mpaka wake na kuwaacha madereva wa malori na wakazi wengine wa Tunduma na hofu ya kuendelea kuporomoka kiuchumi