Virusi vya corona: Je, dawa ya mitishamba kutoka Madagascar inaweza kutibu corona?

Rais wa Madagasca ametangaza dawa ya kunywa ya mitishamba inayotokana na mmea wa pakanga pamoja na mimea mingine inayoweza kutibu maambukizi ya virusi vya corona.

Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema hakuna ushahidi wa kisayansi unaothibitisha kuwa dawa hiyo inaweza kumkinga mtu na virusi vya corona au ni dawa salama kwa matumizi.