Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Coronavirus: Je agizo la kuwa umbali wa mita moja litatekelezwaje katika mitaa ya mabanda Afrika?
Kuna wagonjwa wachache wa Covid-19 barani Afrika ikilinganishwa na maeneo mengine duniani.
Lakini Shirika la Afya Duniani limeonya bara hilo kujiandaa kwa hali mbaya zaidi.
Serikali katika kanda tofauti za Afrika zimebuni masharti makali kama vile kufunga shule na kudhibiti matembezi.
Hatahivyo katika makaazi ya mabanda ambayo yanakaliwa na mamilioni ya watu katika mazingira ya msongamano mkubwa, wengi wao wanahofia ni vigumu kukaa mbali na mwingine au kujitenga.