Mzozo wa Syria: Baba amfundisha mwanae kuyacheka mabomu kukabiliana na dhiki ya vita
Mashambulio ya anga na mabomu yalimfanya baba wa Syria Abdullah Mohammad kubuni njia mpya ya kumsaidia binti yake kuishi na sauti za vita: Kicheko. Mzozo unaoendelea umeifurusha familia yao katika mji wa Saraqib kaskazini mashariki mwa Syria, na kumlazimisha kuishi katika nyumba ya rafiki yake pamoja na binti yake Sarmada.