Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Nini chanzo cha moto Australia na athari zake ni zipi kufikia sasa?
Moto wa nyikani umeua watu 25 na mamia ya wanyama nchini Australia. Moto wa aina hii porini hutokea kila mwaka lakini msimu huu umekuwa mkubwa kupita kiasi.
Moto huo ulioanza mwezi Septemba mwaka jana, unaendelea kuwaka kuelekea mashariki na pwani ya kusini.
Nini chanzo cha moto huu na athari zake kufikia sasa?